Timu zilizowasili CECAFA Tusker Challenge Cup

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura

TIMU zinazoshiriki CECAFA Tusker Challenge Cup zinaendelea kuwasili Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano hayo yatakayoanza Novemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo kwa vyombo vya habari ni kwamba; Somali na Djibouti tayari zimeshawasili. Ikifafanua zaidi taarifa hiyo iliyosainiwa na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura inasema timu hizo zilitua nchini jana mchana kwa nyakati tofauti.

Wambura alisema ratiba ya ujio wa timu nyingine na sehemu zitakapofikia ni kama ifuatavyo; Burundi Nov 23rd 1545hrs RwandAir – Lunch Time Hotel (Ubungo), Djibouti Nov 22nd 1320hrs Ethiopian Airlines – Wanyama Hotel (Sinza) na Ethiopia Nov 24th Ethiopian Airlines – Johannesburg Hotel (Sinza).

Kenya Nov 27th Kenya Airways – Rungwe Hotel (Kariakoo), Malawi Nov 27th Air Malawi – Rombo Green View Hotel (Sinza), Rwanda Nov 23rd 1545hrs RwandAir – Rungwe Hotel (Kariakoo), Somalia Nov 22nd Kenya Airways – Wanyama Hotel (Sinza) na Sudan Nov 23rd 1320hrs Ethiopian Airlines – Marriot Hotel (Mabibo External).

Tanzania – Rainbow Hotel (Morogoro Rd), Uganda Nov 23rd 1600hrs Air Uganda – Royal Valentino Hotel (Kariakoo), Zanzibar Nov 23rd by boat- afternoon – Rombo Green View Hotel (Sinza).

Viwanja vya mazoezi kwa ajili ya timu zinazoshiriki michuano hiyo ni; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (viwanja viwili), Shule ya Sekondari Loyola na Uwanja wa Karume.