China yaikopesha Tanzania mkopo nafuu

Waziri wa Fedha wa Tanzania Mustafa Mkulo (kushoto) na Makamu Waziri wa Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Jiang Yaoping (kulia) akibadilishana hati ya mikataba mitatu (3) ya mikopo isiyo na riba yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 89.8 na barua ya msaada wa ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere kwa thamani ya Dola milioni 5.6 leo jijini Dar es Salaam .

Makamu Waziri wa Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Jiang Yaoping (kulia) akitoa hotuba jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kutia saini na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto) hati ya mikataba mitatu (3) ya mikopo isiyo na riba yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 89.8 na barua ya msaada wa ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere kwa thamani ya Dola milioni 5.6 leo jijini Dar es salaam .

Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Serikali ya Watu wa China wakiwa katika mkutano jana jijini Dar es Salaam na wenzao wa Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es Salaam

Makamu Waziri wa Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Jiang Yaoping(kulia) akitoa zawadi kwa Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto) leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutia saini hati ya mikataba mitatu (3) ya mikopo isiyo na riba yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 89.8 na barua ya msaada wa ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere kwa thamani ya Dola milioni 5.6 leo jijini Dar es Salaam .