Ofisa Elimu wa Sekondari za Wilaya ya Iringa, William Mkangwa akikata utepe kuashiria kupokea msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kwa kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii 'Vodacom Foundation' kwa ajili ya shule ya sekondari ya Lipuri, iliyopo kata ya Kalenga mkoani Iringa, wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule, Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya kusini Jackson Kiswaga, Diwani wa kata ya Kalenga Ameria Galinoma na Giwani Viti Maalum, Shakila Kiwanga.
Wazee wa kabila la Kihehe, kata ya Kalenga mkoani Iringa wakimpa heshima ya kichifu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga kwa kumkabidhi mkuki baada ya kumvisha vazi la mgorole ikiwa ni heshima kubwa kwa mkoa huo wakati walipofika kukabidhi madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 29 katika Shule ya Sekondari ya Lipuri mkoani humo.