Watanzania waishio Ujerumani waanza sherehe za miaka 50 ya Uhuru

Nembo ya miaka 50 ya Uhuru ya Noma Africa Bend.

Shangwe kuanzia Munchen hadi Berlin

WATANZANIA waishio nchini Ujerumani wanaanza kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara kwa vishindo na shangwe zisizo na mfano. Mambo yataanza siku ya Jumamosi, Desemba 3 mwaka huu ambapo Ngoma Africa Band itafanya onesho lake kuzindua mjini München, mtaa wa Siebold Str, 11, majira ya saa 10 alhasiri.

Na usiku bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi ‘Ngoma Africa’ inatarajiwa kutumbuiza katika sherehe hizo za kihistoria zitahamia mjini Berlin, ambako ndio makao makuu ya Ujerumani, kuanzia siku ya Desemba 9, 2011. Mji huo utatingishika na sherehe hizo siku ya Jumamosi Desemba 10, 2011, hii ndiyo siku ambayo Watanzania na marafiki zao wakiwemo wahisani watajimwaga uwanjani kusherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Bendi ya muziki kikosi kazi cha NGOMA AFRICA a.k.a FFU ambacho kinatazamiwa kumwaga burudani ya muziki kitakuwepo uwanjani kwenye usiku huo usiokucha. Siku hiyo pia Ngoma Africa Band itatamba na CD mpya ya “Shangwe 50 Uhuru Anniversary” ambayo imeshaanza kutingisha vituo mbalimbali vya radio ndani na nje ya Tanzania. Wimbo huu pia unasikika kupitia; www.ngoma-africa.com
Watanzania tujitokeze kwa wingi