Nukuu ya leo; ‘Akutukanae hakuchagulii tusi’

Nembo ya Miaka 50 ya Uhuru

JUZI Bungeni msemaji wa kambi ya upinzani, katika mjadala wa Muswada wa Kuunda Tume ya Kukusanya Maoni alisema Rais ni dikteta. Ama kweli “akutukanae hakuchagulii tusi” kama ulivyo msemo wa Kiswahili. Hivi mimi kweli ni dikteta? Kwa jambo lipi? Hivi ndugu zangu Rais dikteta anatoa uhuru mkubwa kama uliopo sasa wa vyombo vya habari na wa watu kutoa maoni yao? Kama mimi ningekuwa dikteta kweli nina hakika hata yeye asingethubutu kusema hivyo na kama angethubutu basi mpaka sasa asingekuwa anatembea kwa uhuru. Mimi ninachofahamu ni kuwa nasemwa kwa kuwapa watu, vyama vya siasa na vyombo vya habari uhuru mkubwa mno ambao watu wanaona unatumika vibaya kusema maneno yasiyokuwa na staha au hata matusi, fitina na kupandikiza chuki katika jamii. Labda, nijaribu kuwa dikteta kidogo watu waone tofauti yake. Naamini kungekuwa na malalamiko makubwa zaidi ya haya.-Maneno haya yalisemwa na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya Novemba 18, 2011 kwa wazee wa Dar es Salaam.