Na Mwandishi Wetu
MAKOCHA wa Timu za Taifa la Tanzania na Chad wametaja vikosi vya wachezaji ambao muda mfupi ujao wataingia uwanjani katika mtanange wa marudiano ya mechi za kufuvu fainali za Kombe la Dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura kwa vyombo vya habari mapema leo-amesema tayari makocha wote wametaja vikosi vyao pamoja na wachezaji wa akiba.
Alisema katika mchezo huo unaotarajia kuanza majira ya saa kumi jioni, Timu ya Taifa Stars ya Tanzania itawakilishwa na
goli kipa Juma Kaseja (1), Shomari Kapombe (2), Idrissa Rajab (15), Juma Nyosso (4), Aggrey Morris (6), Shabani Nditi (19),
Thomas Ulimwengu (20), Henry Joseph (17), Mbwana Samata (10)
Nizar Khalfan (16), pamoja na Mrisho Ngassa (8).
Wambura alisema wachezaji wa akiba wa Stars ni: Mwadini Ally (18), Erasto Nyoni (12), Hussein Javu (23), Mohamed Rajab (11)
Ramadhan Chombo (21), Abdi Kassim (13), Nurdin Bakari (5)
John Bocco (9), Juma Jabu (3), pamoja na Godfrey Taita (7)
Kwa upande wa Chad itawakilishwa na Brice Mabaya (1), Sylvain Doubam (5), Massama Asselmo (15), Armand Djerabe (4), Yaya Karim (2), Herman Doumnan (6), Ferdinand Gassina (17), Ahmat Mahamat Labo (10), Ezechiel Ndouassel (11), Hassan Hissen Hassan (7) na Dany Karl Marx (9).
Aidha wachezaji wa akiba ni, Cesar Abaya (12), Wadar Igor (13)
David Mbaihouloum (8), Dillah Mbairamadji (16), Djingabeye Appolinare (3), Rodrigue Casmir Ninga (18), Mahamat Habib (14), Marius Mbaiam, Abakar Adoum, Jules Hamidou na Ekiang Moumine.