Mbunge atoa milioni 6.5/- kwa waathirika

MBUNGE wa Igunga, Rostam Aziz ametoa pole ya Sh milioni 6.5 kwa wananchi walioathiriwa na mvua kubwa wilayani hapa WAATHIRIKA wa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Janga hilo lilisababisha kaya 66 kukosa mahali pa kuishi katika kitongoji cha Hani wilayani hapa.

Mbunge huyo alikwenda kuwatembeloea waathirika hao katika zahanati ya Kata ya Igunga jana.

Alisema alitoa fedha hizo kwa kaya 13 ambazo zina watu 103 ambao hawana makazi hadi sasa.

Kila kaya itapata takriban Sh 500,000 kukarabati nyumba zilizoezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali, alisema.

Wanahifadhiwa katika zahanati hiyo wakati halmashauri itasaidia kwa mahijati mengine ya binadamu.

Mbunge huyo alisema katika tukio hilo hakuna mtu aliyepoteza maisha bali majeruhi wapatao 10
wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga