Makamau wa Rais Dk Bilal azindua Kampeni ya Chanjo ya Surua na Polio

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimpa tone la dawa ya Chanjo mtoto, Renatha Faustine (1) wakati wa alipokuwa akizindua Kampeni ya Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Novemba 12, 2011. Aliyembeba mtoto ni mama wa mtoto huyo, Selina Hando Mkazi wa Moshono Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Novemba 12, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Watoto wa Shule za Msingi, wakipita mblele ya jukwaa la mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, na mabango yenye ujumbe wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Novemba 12, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais DK. Gharib Bilal akipata maelezo kutoka kwa mtoa huduma wa afya kabla ya kutoa matone ya Vitamin A wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa ya Surua,utoaji wa matone ya Polio, Vitamin A na dawa ya minyoo uliofanyika leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume, Arusha Picha na MAGRETH KINABO – MAELEZ0