MCHEZO wa maadalizi ya kufuzu mechi za makundi kuelekea fainali za kombe la Dunia kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Timu ya Taifa ya Chad umemalizika muda mfupi uliopita na Tanzania kuibuka mshindi.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya mjini N’Djamena, Stars imefanikiwa kushinda mabao mawili kwa moja la Chad. Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata mara baada ya mchezo huo, ni kwamba Tanzania ndio iliyoanza kufunga katika kipindi cha kwanza na baadaye chadi kusawazisha.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilikuwa 1-1. Stars walipata goli la pili katika kipindi cha pili goli ambalo lilidumu hadi mwisho wa dakika 90 za mchezo huo.