Na Danstan Mhilu
MUUNGANISHO wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) Mkoa wa Ruvuma umetoa mafunzo kwa waendesha mashine za kukamua mafuta ya alizeti mjini hapa. Mafunzo hayo yaliyofanyika Ofisi za Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), huku miongoni mwa wanavikundi waliopata mafunzo hayo wakiwa ni wana vikundi wapatao 20.
Awali akifungua mafunzo hayo Kaimu Meneja wa SIDO, Ruvuma, Athur Ndedya aliwasihi wana vikundi kupokea mafunzo hayo pamoja na kuyafanyia kazi yale ambayo wameelekezwa na wataalamu ili kuepuka usumbufu na hasara wakati wakuendesha mashine zao.
”Nawasihi sana kumsikiliza fundi kwa umakini ili kuchukuwa tahadhari ya changamoto ya matumizi ya mashine”. Hata hivyo amesema endapo hawatazitunza katika hali ya usalama na usafi MUVI na SIDO hawata sita kuondoa mashine hizo nakuzipeleka katika vijiji vingine ambavyo vipo ndani ya mradi ambavyo havikufungiwa mashine.
Vikundi vilivyofungiwa mashine hizo ni Kilosa na Mkako kwa wilaya ya Mbinga, Matimira, Lundusi, Mpandangindo na mtyangimbole kwa Wilaya ya Songea Vijijini wakati kwa wilaya ya Namtumbo ni Hanga na Utwango. Vijiji ambavyo havikufungiwa mashine ni Kigong, sera, Amani makolo na Mkalole kwa Wilaya ya Mbinga.
Vingine ni Liganga kwa wilaya ya Songea vijijini, msindo kwa Wilaya ya Namtumbo moja ya vigezo vilivyotumika kufunga mashine hizo katika maeneo yaliyo olozeshwa ni kutokana na swala la ukaribu wa kufikika kwa vikundi vingine vinavyo zunguka eneo hilo kwa maana senta.
Fundi aliyefunga mashine hizo ni Mussa Mussa kutoka kampuni ya Survivo General Enterprises ya mjini Iringa akitoa mafunzo hayo aliwatahadharisha kuwa makini waendeshapo mashine hizo kwa usalama wao na mashine kwa ujumla.
Akianisha vitu ambavyo wanatakiwa kufanya ni pamoja na kuvaa ovaroli, kutokuvaa mikufu, kuto kunywa pombe au kuvuta sigara wakati wakuendesha mashine hizo kuwepo kwa kisanduku cha huduma ya kwanza nakuto sita kuwa taarifu MUVI endapo yatatokea matatizo ambayo yapo chini ya uwezo wao.
Naye mratibu wa mradi wa MUVI mkoa wa Ruvuma Nema Munisi akichangia mada katika mafunzo hayo aliwasihi kuzingatia kile walicho jifunza ili mashine hizo ziwafae kwa sasa na baada ya mradi kuisha.
”Tumieni na kuzitunza ili ziwafae mradi una mwisho lakini mkizitunza zitawafaa hata kizazi kijacho cha msingi nikuzingatia yaliyozungumzwa na fundi nakuyafanyia kazi na endapo kuna tatizo lililo nje ya uwezo wenu muwasiliane na fundi”.
MUVI imefunga mashine tano katika kijiji cha kilosa, mkako, Lundusi, Hanga na matimira, imewza kusaidia vikundi vingine ambavyo ni Utwango, Mtyangimbole na mpandangindo ambavyo mashine wamepatiwa DADPS lakini MUVI inawasaidia kufunga mashine hiyo wakati ile ya Utwango ikifungwa na SIDO.
Kwa picha zaidi, tafadhali bofya hapa: http://www.thehabari.com/matukio/muvi-yatoa-mafunzo-kwa-waendesha-mashine-za-kukamua-mafuta-ya-alizeti-2