CAF kutoa leseni za ukocha daraja ‘C’

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura

KOZI ya ukocha kwa ajili ya kupata leseni za daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanzia kesho (Novemba 7 mwaka huu) hadi Novemba 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TFF kupitia kwa Ofisa Habri wake, Boniface Wambura amesema makocha 30 ndiyo wanaoshiriki kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi wanne; Jan Poulsen kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Kasimawo Laloko (Nigeria) na Sunday Kayuni wanaotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Kim Poulsen kutoka Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU).

Amesema washiriki wa kozi hiyo ni Abdul Nyumba, Absolom Mwakyonde, Ahmed Mumba, Christopher Eliakim, Dismas Haonga, Edward Hiza, Eliasa Thabit, Emmanuel Massawe, Fulgence Novatus, Gabriel Gunda, Gideon Kolongo, Haji Amir na Hassan Banyai.

Aliwataja wengine ni Juma Mgunda, Jumanne Ntambi, Keneth Mkapa, Leonard Jima, Maarufu Yassin, Maka Mwalwisi, Mecky Maxime, Mohamed Tajdin, Mussa Furutuni, Mussa Kamtande, Peter Mhina, Richard Kabudi, Sebastian Nkoma, Stephen Matata, Tiba Mlesa, Wane Mkisi na Wilfred Kidau.