Ijue chai ya Kichina inayoondoa sumu mwilini

Dorothy Hamilton (aliyekaa na T.Shirt) Mtaalam Mshauri wa dawa za China akitoa maelezo kwa baadhi ya wateja ambao wanatembelea banda la Kampuni yao katika Viwanja vya Kichina. Kulia waliosimama ni wateja wakisikiliza kwa makini.

WATAALAMU wa masuala ya afya wanasema katika vyakula na vinywaji mbalimbali tunavyokula na kunywa kila siku vingi vina kiasi fulani cha sumu ambazo mara nyingine huweza kuleta madhara mwilini.

Kama hivyo ni kweli kwa mujibu wa wataalam wa masuala ya afya kila binadamu anakiasi fulani cha sumu ambacho anakipata kutokana na vyakula na vinywaji anavyokunywa. Ipo sumu ambayo tunaipata kutoka kwenye vyakula na vinywaji vyenye kemikali na hata kwenye mafuta mbalimbali.

Huenda zikawa zipo njia anuai za kitaalamu ambazo zinaweza kutumika kutoa sumu hiyo mwilini. Lakini Dorothy Hamilton mmoja wa wataalam wa ushauri wa dawa za asili za Kichina nchini anasema kipo kinywaji mithili ya chai ambacho kinatoa sumu zote mwilini.

Akifanya mahojiano na dev.kisakuzi.com kwenye Maonesho ya Wajasiriamali Wanawake yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja; nasema kinywaji hicho kinaitwa, TIENS. Anafafanua kuwa kinywaji hutumika kunywewa kama chai kwa mtu yeyote endapo atakuwa tayari kukitumia. Anasema baada ya muhusika kutumia kinywaji hicho kikiwa cha moto kama chai muda huo huo huanza kutoa sumu kupitia kutoka jasho ama kwa haja kubwa kawa inavyokuwa kawaida.

Je, wataka kujua zaidi kuhusu chai tiba hiyo. Fanya mawasiliano kwa kutumia njia hii; 0658904714