Mtanzania Flaviana Matata atwaa tuzo ya mwaka

Flaviana Matata katika moja ya pozi zake za kiuanamitindo zinazowapagawisha watu kila kona

Flaviana Matata, Mtanzania ambaye amekuwa akitengeneza vichwa vya habari katika majariba mbalimbali ya masuala ya ubunifu duniani, ameendelea kuing’arisha Tanzania katika masuala ya mitindo baada ya kutwaa tuzo ya Mwanamitindo bora wa mwaka huko nchini Nigeria.

Tuzo hizo zilizotolewa na jarida maarufu la mitindo la Arize Magazine la nchini Nigeria, zilishuhusia Klûk CGDT, akitwaa tuzo ya mbunifu bora wa mwaka, Maki Oh akitwaa tuzo ya mbunifu bora anayechipukia.

Tuzo hizo zilitolewa hivi karibuni wakati wa wiki ya mitindo iliyoandaliwa na jarida hilo ambapo mbunifu Mustaffa Hassanali aliwakilisha Tanzania kwa upande wa wabunifu. Jukwaa Huru Media, kwa niaba ya wadau wake wote kote waliko duniani, tunapenda kumtakia kila lakheri Flaviana Matata katika kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye nyanja ya mitindo.