Uingereza kupambana na watekaji wa meli Somalia

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema kuwa meli zilizosajiliwa Uingereza zinaweza kuwa na walinzi wa kujihami ili kujikinga na maharamia.

Waziri mkuu huyo alitoa taarifa hizo alipokuwa akihojiwa na Shirika la Habari la BBC, na kuongeza kuwa anataka kushughulikia zaidi tishio linalokabili meli katika pwani ya Somalia – ambako meli 49 zilitekwa na maharamia mwaka jana.

Hivi sasa sheria hairuhusu walinzi kubeba silaha kwenye meli za Uingereza, lakini Bwana Cameron alisema anakusudia kubadilisha sheria hiyo: “Sasa tutasema kwamba meli zilizosajiliwa Uingereza, zitaweza kuwa na walinzi wenye silaha katika meli hizo zikitaka.

Mimi nataka kuhakikisha kuwa maharamia wengi zaidi wanafikishwa mahakamani; na nataka tuitazame zaidi nchi hii ya Somalia iliyoharibika…na vipi tunaweza kujaribu kushughulikia sababu za utekaji nyara, uharamia, kikombozi, na matatizo yote yanayotokana na nchi hii iliyochafuka.”

-BBC