Nape ajikoroga, aitwa mahakamani Arusha

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye

Na Janeth Mushi, Arusha

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imemuita Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye kufika na kutoa ushahidi juu ya madai yaliyotolewa mahakamani hapo.

Jaji Aloyce Mujulizi ambaye anasikiliza kesi ya kupinga matokeo ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA) jana mjini hapa aliamuru kiongozi huyo kuitwa mahakamani pamoja na Mhariri wa gazeti la Nipashe kuthibitisha taarifa zilizotolewa na gazeti hilo.

Mujulizi alitoa amri hiyo baada ya Wakili anayemtetea Mbunge huyo Method Kimomogolo, kutoa gazeti la Nipashe mahakamani hapo toleo namba 57162 la Oktoba 9, 2011 kama kielelelezo.

Kimomogolo akinukuu maneneo aliyoyasema katibu huyo alisema kuwa, wana uhakika wa kushinda kesi dhidi ya Mbunge Godbless Lema(CHADEMA) na kuchukua jimbo hilo uchaguzi utakapokamilika”alinukuu gazeti hilo.

Kimomogolo aliieleza mahakama hiyo kuwa kutokana na kauli ya katibu huyo Lema, viongozi wa Chadema na wafuasi wake wameingiwa wasiwasi juu ya uendeshwaji wa kesi hiyo.

“Mahakama ina uwezo wa kumdhibiti yoyote anayeingilia taratibu za Mahakama kama Nape, hivyo aitwe atueleze kwa nini asipelekwe jela kwa kuingilia uhuru wa mahakama? aadhibiwe kwa mujibu wa sheria kwa kuingilia uhuru wa mahakama,” alisema Method.

Kufuatia madai hayo Kimomogolo alimweleza Jaji huyo kuwa Jaji Mkuu ateue Majaji wengine watano wa kusikiliza shauri hilo kwa madai kuwa shauri hilo limeiibua mambo mengi mapya ambayo hayajawahi kutolewa maamuzi katika mahakama hiyo wala mahakama ya rufaa.

“Ili haki ionekane kuwa imetendeka uone busara kujiondoa katika kusikiliza shauri hili” aliongeza Kimomogolo kwa madai kuwa mteja wake hana imani na Jaji huyo ambaye huenda ikawa ametishiwa au amewahakikishia wadai kuwa wanashinda kesi hiyo.

Kwa upande wake wakili wa wadai Alute Mughwai, alimwomba jaji huyo kutupilia mbali maombi ya wakili wa utetezi kwa madai kuwa maombi ya Kimomogolo yamewasiliswha mahakamani hapo kwa lengo la kuchelewesha usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo ikiwa ni pamoja na kutaka Jaji ajiondoe kusikilzia kesi hiyo.

“Masuala ya kisheria anayodai Kimomogolo ambayo yanbishaniwa katika shauri hili hayapo yaliyobaki ni masuala ya ushahidi,” alisema Alute.

Awali Alute alisema sheria za uchaguzi 2010 zinasema kesi za uchaguzi zinatakiwa kusikilizwa katika mahakama ya wazi, hivyo suala la vipaza sauti mahakamani hapo msajili alizingatie ili wananchi wapate haki yao kimsingi.

Kufuatia maombi hayo Mujulizi alikubaliana na hoja zilizotolewa na Kimomogolo na kuahirisha shauri hilo hadi Novemba 16 mwaka huu ambapo Katibu huyo na Mhariri wa Gaseti la Nipashe watatakwia mahakamani hapo kuthibitisha kauli zilizochapishwa katika gazeti hilo kama ni za kweli
au la.

Aidha Mujulizi akiahirisha shuri hilo alisema kuwa suala la yeye kujiengua katika usikilizaji wa kesi hiyo atalitolea maamuzi Novemba 16.

Awali mahakamani hapo kulitokea mvutano makali baina ya Mkuu wa polisi wailaya ya Arsuah Zuberi Mwombeji na Lema baada ya Mkuu huyo kuwazuia wafuasi wa chama hicho waliokwua wamefika mahakamani hapo.

Aidha kutokana na eneo hilo la mahakama kuwa na ulinzi mkali wa polisi wakiwemo Kikosi Cha Kuzuia Ghasia (FFU), ambapo Zuberi na Mbunge huyo walikuwa katika mabishano ambayo lema alikuwa akitaka wafuasi hao kuingia mahakamani wote.

Kufuati shauri hili kuahirishwa juzi kutokana na wingi wa watu, Zuberi ambaye alikuwa akimwelewesha Mbunge huyo na kumweleza kwua polisi kazi yao ilikuwa ni kuwapanga watu katika chumba cha mahakama na wale wanaokosa nafasi za kukaa kubaki nje jambo ambalo mbunge huyo alikuwa akilipinga na hatimaye kukubaliana na hali hiyo.