Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Uhuru One, Mihayo Wilmore, kuhusu matumizi rahisi ya kompyuta ndogo na mpango wa kuzisambaza na kuwawezesha wanafunzi wa Tanzania kutumia kompyuta hizo, wakati wakati akikagua banda la maonyesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Na Mwandishi Maalumu, Geneva, Switzerland
KAMPUNI ya Uhuru One inaangalia uwezekano wa kutoa mafunzo ya matumizi rahisi ya kompyuta ndogo (laptop) mpango ambao utakwenda sambamba na kuwawezesha na kuwasambazia wanafunzi wa Tanzania ili waweze kuzitumia kompyuta hizo.
Taarifa hiyo imetolewa le mjini Geneva, Switzerland na Meneja wa Uhuru One, Mihayo Wilmore, alipokuwa akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, kuhusiana na matumizi rahisi ya kompyuta hizo, ndani ya banda la maonesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa Mawasiliano wa Kampuni ya Qatar Assistive Technology Center, Ahmed Habib, ambaye ni mlemavu, wakati alipotembelea Banda la maonyesho la kampuni hiyo katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR