Serikali yawasaka wafanyabiashara haramu wa madini

Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja

Na Janeth Mushi, Arusha

SERIKALI mkoani hapa leo inafanya msako kuwatafuta wafanyabiashara
wadogo (ma-bloker) wanaofanya biashara hiyo bila ya leseni. Wafanyabiashara wanaoendesha biashara hiyo bila taratibu watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Erick Mpesa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa. Amesema msako huo utakuwa wa siku tatu ambapo utaanzia mjini Arusha na baadaye mikoa ya Kilimanjaro na Manyara.

“…leo msako utaanza rasmi na watakaokamatwa watafikishwa
mahakamani kwani wafanyabiashara walifahamishwa kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010 kifungu 18 (4) kuwa mtu yoyote ambaye anamiliki madini kinyume na sheria akithibitika adhabu yake itakwua faini isiyopungua milioni 10 aina kifungo kisichozidi miaka 3 au vyote kwa pamoja,” alisema

Amesema kuwa awali Serikali iliiagiza ofisi hiyo kukata
leseni kwa wafanyabiashara wadogo wa madini mkoani hapa baaada ya
kubaini kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo
bila leseni na Mei mwaka huu ofisi hiyo ilitoa mafunzo kwa
wafanyabiashara hao juu ya uvunjaji wa sheria kwa kufanya biashara
bila leseni.

Alisema kuwa tathmini ilionyesha kuwa wafanyabiashara 400 walikwua
wakijihusiaha na biashara hiyo pasipo kuwa na leseni ila baada ya
serikali kwuapa muda tangu Mei mwaka huu hadi octoba 21 ambapo hadi
hivi sasa ni wafanyabiashara 250 pekee waliokata leseni hizo.

“Hadi jana tumeweza kukata leseni 130 za broker na kuwa kuwa
tumeruhusu watu wawili kuchangia leseni moja leseni hizo zimebeba
jumla ya ma broker 250,” alifafanua

Mpesa aliongeza kwua mbali na kuhakikisha kuwa wanaojihusisha na
biashara hiyo kwa mujibu wa sheria msako huo pia una lengo la
kuhakikisha walaojihusisha na biashara hiyo ni Watanzania pekee.

“Sheria ya madini inazuia watu ambao si Watanzania kujihisisha na
biashara ya madini kwa upande wa wafanyabiashara wadogo na ndiyo
maaana wanapokuaja kuomba leseni lazima waje na vitambulisho vyao vya kupiga kura,” alisema.

Alifafanua kuwa msako huo utaweza kuwasaidia Watanzania bila
kuingiliwa na watu ambao siyo nchi hii na iwapo watu ambao si raia wa Tanzania wanataka kufanya biashara ya madini, wanatakiwa kuomba leseni kubwa za biashara “Dealer licence” ambayo gharama yake ni 515,000 huku leseni za wafanyabiashara wadogo zikiwa ni 115,000.