Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa Timu za Vijana Tanzania, Kim Poulsen ametaja kikosi cha Timu ya Vijana wa Chini ya Miaka 17. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura (pichani) jana; amesema Poulsen amewataja wachezaji 14 ambao wanatarajia kuondoka nchini Oktoba 27 kuelekea Johannesburg Afrika ya Kusini. Amesema timu hiyo itaanza mazoezi leo katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Wachezaji 14 na wa akiba wawili ni pamoja na;- Hamad Juma, Peter Manyika, Mgaya Abdul, Ismail Gambo, Miraji Selemani, Basil Seif
Mohamed Hussein, Hussein Ibrahim, Selemani Bofu, Mudathiri Abbas
Mohamed Haroub, Faridi Shah, Mbwana Hassan, Joseph Lubasha
Wachezaji wa akiba waliotajwa ni Pascal Matagi na Salvatory Nkulu.