Viongozi wa EU kufikia mwafaka wa sarafu ya euro

KANSELA wa Ujerumani na Rais wa Ufaransa,

KANSELA wa Ujerumani na Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy,

,

KANSELA wa Ujerumani na Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy wamefanya kikao maalum pamoja na viongozi wa mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya. Mkutano huo umefanyika ikiwa ni siku nne kabla ya kikao maalum kitakachoyajadili masuala ya fedha na mitikisiko katika eneo linalotumia sarafu ya euro.
Duru zinaeleza kuwa, Rais wa Umoja wa Ulaya, Herman Van Rompuy, mwenzake wa Kamisheni ya Umoja huo, Jose Manuel Barroso, Mkurugenzi Mkuu wa Benki Kuu ya Italia aliye pia rais mtarajiwa wa Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya, Mario Draghi walikihudhuria kikao hicho maalum.
Kwa upande wake, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, aliyekuwako Frankfurt kuhudhuria sherehe maalum za kumuaga rais wa Benki Kuu ya Ulaya, Jean-Claude Trichet, anayeondoka, alisisitiza kuwa ni wajibu wao kufanya kila linalowezekana kuilinda sarafu ya euro.
Jean- Claude Trichet anaondoka rasmi Novemba Mosi na Maro Draghi wa Benki Kuu ya Italia ndiye atakayeshika hatamu. Azma ya mkutano huo wa jana jioni ni kuzipunguza tofauti zilizopo kati ya viongozi wa Umoja wa Ulaya kabla ya kikao cha kilele cha Jumapili kufanyika mjini Brussels nchini Ubelgiji.

-DW