Hizi Hapa Sera za Fredrick Mwakalebela Mgombea Urais TFF

Fredrick Mwakalebela 

 

MGOMBEA Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela ametaja mambo kumi atakayo fanya katika kuinua mpira hapa nchini kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa TFF.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati uzinduzi wa kampeni yake Mwakalebela amesema kuwa kwa kuanza ataanza na Utawala bora kwa Kuweka misingi ya wazi katika mapato na matumizi ya TFF, Kuzifanya kamati za TFF kuwa huru na kufanya kazi bila kuingiliwa, uingalia upya Agenda ya kupunguza idadi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ili tuweze kupanua wigo wa wadau wa mpira wa miguu kutuwakilisha kwa wingi katika mkutano mkuu.
amesema kuwa pia ataweza kusimamia matakwa ya katiba ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kwa kufanya vikao na mikutano inayotambuliwa kikatiba, kuwa na vyombo imara vya usimamizi ndani ya shirikisho ili kuleta matokeo chanya yenye ufanisi katika soka.
Mwakalebela amesema ataweza kusaidia Timu za Taifa, wanaume, Wanawake na Vijana kwa Kuwa na makocha wenye viwango vya juu ikiwa ni pamoja na Kurudisha hamasa kwa watanzania kuzipenda timu za Taifa kwa kuongeza idadi kubwa za wachezaji wa ndani kucheza nje ya nchini pamoja na kucheza FIFA date zote na Kuziweka timu kambini kwa wakati.
aidha katika mpango huu  wa pili ataweza Kuanzisha na kusimamia Academy nyingi Tanzania kwa kuhakikisha timu zinapata mechi nyingi za kirafiki na kimataifa kuandaa mashindano ya kimataifa Kuwa na mfadhili wa kugharimia mpango kazi wa timu za Taifa.

 

Katika mpango wake wa tatu Mwakalebela amesema atashirikiana naVilabu kwa Kupitia upya mikataba ya sasa ili kuiboresha na kuleta tija katika vilabu pia ameadhimia kuongeza idadi ya mashindano ili kuongeza ufanisi kwa wachezaji na Taifa kwa ujumla.
Ameongeza  ataweza kuboresha kanuni zetu kuwa zenye tija na ufanisi hili kuongeza mapato ya vilabu kwa kuifanya Bodi ya Ligi kuwa huru nakuweza kuboresha viwanja vya mashindano pamoja na kuongeza idadi ya wadhamini kwa kufanya mpira kuwa starehe na biashara.

 

Katika kusaidia Vyama vya Soka vya Mikoa   Mwakalebela amesema kuwa atafanikisha kupatikana kwa   vitendea kazi kama mipira,kompyuta,printers na thamani za ofisini na kuwawezesha  kuwapatia Wadhamini wa kudumu kwa ajili ya ofisi kujiendesha na  kuwapatia ruzuki za kila mwezi kwa shughuli za chama kwa kuongeza idadi ya mashindano mikoaniKuboresha viwanja na ofisi za mikoani kuwapatia viongozi mafunzo ya kuwajengea uwezo ndani na nje ya nchi.


Katika kusaidia Vyama Shiriki Waamuzi, Tiba Michezo, Waamuzi, Tiba Michezo, Makocha, Wanawake, Sputanza kwa  Kutoa Mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili kuwajengea uwezo, Kuwapatia ruzuku kwa ajili ya shughuli za kila siku na kuwapatia wadhamini kwa kuwapatia vitendea kazi.

 

Katika kuboresha Sekretarieti Mwakalebela amesema atawezesha Sekretarieti kuwa na watendaji wenye weledi na uwezo katika maeneo yao ya kazi kwa

 

Kuajiri watendaji kwa kuzingatia sifa na vigezo katika nafasi husika.
Kuongeza uadilifu katika utendaji kazi. Kusimamia watendaji waweze kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia uhitaji wa wadau wa soka nchini.
Kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo ndani na nje ya nchi.

 

Katika Mahusiano na Wadau Mwakalebela amesema
Ili kupata mafanikio chanya katika maendeleo ya soka ni lazima kuhakikisha wadau wanashirikishwa ipasavyo, hivyo nitahakikisha natambua nafasi ya wadau na kushirikiana nao, Serikali pamoja na Vyombo vyake, Wachezaji wa sasa na wale wa zamani, Wanahabari, Taasisi, Mashirika na Kampuni mbalimbali, Mashabiki na wapenzi wa mpira, Wadhamini na wafadhili, Wamiliki wa viwanja vya michezo, Watanzania wote kwa ujumla.

 

Katika uwekezaji wa Kitega Uchumi Mwakalebela ametaja kuwa Mafanikio ya mpira yanahitaji rasilimali fedha, kwa kulitambua hilo, nitahakikisha kunafanyika uwekezaji wa jengo la kisasa la kitega uchumi katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume ili kuweza kusaidia ufanikishaji.
Amesema Uwezeshaji wa ruzuku kwa wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu katika ngazi mbalimbali kutokana na uhitaji, Mafunzo kwa wanachama, Vitendea kazi kwa wanachama, Uboreshaji wa ofisi za TFF kuwa zakisasa zaidi.

 

Katika kuboresha Bodi ya ligi Mwakalebela amesema Bodi ya Ligi itakuwa huru kwa kuijengea uwezo kwa kuongeza wafadhili na Kuwa na Mpango kazi  ambao utasaidia kuifanya bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi pasipo kuingiliwa.
Katika kuboresha Miundombinu Mwakalebela amesema kuwa kwa Kushirikiana na wamiliki wa viwanja ataweza  kuviboresha hili kuwa na nyasi bandia katika kila kanda kwa kuwa na Viwanja vyenye hadhi na sio kuta tu peke yake.