MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BANDA LA COSTECH MAONYESHO YA NANENANE LINDI

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, HusseinMansour (hayupo pichani), alipotembelea banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kwenye Maonyesho ya Nanenane viwanja vya Ngongo mkoani Lindi leo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu. Maonyesho hayo yatafungwa na Makamu wa Rais leo mchana.

Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour (kushoto), akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, alipotembelea banda la COSTECH.

 

Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la COSTECH katika maonyesho hayo.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni (MARI), Christina Kidulile, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la COSTECH jinsi ya kuotesha mimea kwa kutumia chupa.
 Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Philbert Nyinondi, kushoto akizungumza na wadau wa kilimo jinsi Maktaba ya Taifa ya Sokoine ya Kilimo-SNAL itakavyowawezesha wakulima wa Tanzania kupata taarifa za kilimo kwa njia rahisi.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Patric Ngwediage (wa nne kulia), akiwa na Crew nzima ya COSTECH katika banda hilo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Philbert Nyinondi (katikati) akigawa vipeperushi kwa wakulima ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), vinavyohusu Maktaba ya Taifa ya Sokoine ya Kilimo-SNAL. Kushoto ni Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni (MARI), Christina Kidulile.

 


Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda, akitoa maelekezo kwa wakulima jinsi ya kuotesha miche kwa njia ya chupa.