Na Joachim Mushi, Tanga
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Magembe amewaonya wananchi walio jirani na hifadhi za taifa kuacha mara moja kitendo cha kuchanganya mifungo na wanyamapori kwani kitendo hicho ni hatari kubwa kwa afya za wananchi na mifugo yao. Alisema wanyamapori wana magonjwa mbalimbali na hatari kwa afya zetu hivyo kitendo cha kuchanganya mifugo na wanyamapori huamisha magonjwa kutoka huko na kuingia kwa wananchi wanapokula nyama.
Waziri huyo mwenye dhamana na Maliasili na Utalii alitoa onyo hilo jana jijini Mbea alipokuwa akifungua Mkutano na Semina ya mwaka kwa wahariri na wanahabari waandamizi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA). Alisema kitendo cha wafugaji kuchanganya wanyamapori na mifugo ni changamoto nyingine kubwa, hivyo kuwaomba waandishi wa habari kupitia vyombo vyao kutoa elimu kwa wafugaji. Alisema wanyamapori huwa na magonjwa mengine ambao kwao hayana madhara makubwa lakini yanapoingia kwa mwanadamu huhatarisha maisha yake kiafya.
“…Wananchi kuingiza mifugo yao mbugani hili ni tatizo kubwa, tunaomba mtusaidie…kwanza sheria zetu haziruhusu kabisa suala hili. Tusichanganye mifugo na wanyamapori hii ni hatari tunaweza kubeba magonjwa kule na yakawa na madhara makubwa kwetu…kuna magonjwa kama kimeta, TB na homa za vipindi ambazo zipo kwa wanyamapori zikija kwetu hizi ni hatari,” alisisitiza Profesa Magembe.
Hata hivyo, Waziri Magembe alipongeza juhudi zinazofanywa na wanahabari kupitia vyombo vyao kwani wamekuwa msaada mkubwa kutoa elimu ndani na nje ya nchi. Aliongeza kuwa matokeo ya wanahabari kutumia kalamu zao kutangaza utalii yanajionesha wazi kwa ongezeko la idadi ya watalii kutoka nchi mbalimbali kutembelea hifadhi zetu.
Aidha ameitaka TANAPA kuendelea kushirikiana na wanahabari kwa kufanya semina hizo kila mwaka ili kupata mrejesho juu ya kazi wanayoifanya, kwani vyombo vya habari ni fursa nzuri ya kutoa elimu kwa umma na kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo. Mkutano huo wa siku tatu ulioanza leo Julai 26 unatarajia kumalizika Julai 29, ambapo wanahabari watajifunza na kujadiliana masuala mbalimbali ya utalii na uhifadhi.
Idadi kubwa ya watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani bado wanamiminika kuja nchini Tanzania kutembelea vivutio anuai vya utalii. Alisema hali hiyo imebainika baada ya ziara aliyoifanya kutembelea hoteli mbalimbali za kitalii na kujionea namna zinavyopokea watalii mfululizo, huku baadhi zikiwa zimejaa na wateja kulazimika kuweka oda mapema kabla ya kuanza safari ya utalii.
“…Mimi nimetembelea kabla ya kuja hapa baadhi ya hoteli kwenye maeneo ya utalii kujionea, kweli hoteli baadhi zinawatalii wa kutosha kiasi kwamba zingine zimejaa…mteja ukienda bila ya kufanya ‘booking’ ya chumba huwezi kupata, hawana nafasi pia. Na watalii wanaokuja wanatoka kila upande, kimsingi ujio huo wa watalii kwa wingi ni mafanikio yenu wanahabari,” alisema Waziri Prof. Magembe.
Alisema watu wa kupongezwa ni waandishi wa habari ambao kiasi kikubwa; ningekuwa na kofia hapa ningewavulia kwa heshima na kutambua mchango wenu kwa kazi hii,” alisema.
Hata hivyo alisema bado suala la ujangili dhidi ya wanyamapori ni changamoto japokuwa kwa sehemu kubwa kuna tunaweza kujivunia mapambano na jitihada tulizozifanya kudhibiti hali hiyo. mabadiliko makndiyo wanaotumia kalamu zao kuutangazia utalii wetu.