Mbunge Jimbo la Tanga Ajitosa Sakata la Mgomo wa Daladala

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na madereva wanaofanya safari zao kati ya Masiwani,Magomeni, Majengo na Raskaone Jijini Tanga  waliogoma kutoa huduma kwa siku nzima wakiishinikiza Halmashauri kuikarabati barabara wanazozitumia kutokana na ubovu ambapo Mbunge huyo aliwataka kuendelea shughuli zao wakati kilio chao kikifanyiwa kazi.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani (RTO) Nassoro Sisiwaya akizungumza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza na waansdishi wa habari kuhusu namna halmashauri ilivyoweza kulitatua tatizo hilo mara moja kwa
kupitisha greda kuichonga.
 Kaimu DTO wa wilaya ya Tanga, Imani Raphael akizungumza katika tukio hilo la mgomo wa madereva hao.
Kaimu DTO wa wilaya ya Tanga,Imani Raphael akizungumza na  madereva hao ambapo aliwataka kuendelea na shughuli zao wakati suala lao likishughuliwa na mamlaka
husika.
Diwani wa Kata ya Duga (CUF) Khalid Rashid akizungumza katika mgomo huo
habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.