Wananchi wa Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu wakishirikiana na Mbunge wao na Mwakilishi katika ujenzi wa Taifa wa Soko la Samaki katika ufukwe wa Bahari ya Unguja Ukuu Zanzibar.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said na Mhe Khalifa Salum Suleiman wakikabidhi mabati kwa Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Bi. Sauda Ramadhani, hafla hiyo ya makabidhiano ya Mabati hayo na miti yamefanyika katika viwanja vya Soko hilo Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini.
Wananchi wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa kijiji hicho kuuzia samaki wao.
Wananchi wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa kijiji hicho kuuzia samaki wao.
Kiongozi wa Kijiji cha Tindini akitoa maelezo ya ujenzi wa Soko hilo la Samaki katika ufukwe wa bahari yao litakalotowa huduma ya kuuzia samaki kwa wavuvi katika soko la mnada.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Soko la Samaki katika kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitumia soko hilo kwa shughuli zao za biashara ya samaki na minada kwa wavuvi wanaorudi bahari kuvua.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo kwa Wananchi wa Jimbo lake.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Bi Sauda Ramadhani akizungumza wakati wa hafla hiyo ujenzi wa taifa na kukabidhi mabati na vifaa vya ujenzi wa Soko la Samaki katika Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja.
Wananchi na wavuvi wa kijiji cha Tindini Unguja Ukuu wakimsikiliza mgeni rasmin wakati wa hafla hiyo ya ujenzi wa Taifa na kukabidhi mabati kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Soko hilo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge na Mwakilishi na Wananchi wa Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu baada yas hafla hiyo.
Imetayarishwa na Othman Mapara.