Global peace Foundation Tanzania: Vijana wanaohitimu shule na vyuo waepuke kujiingiza katika matukio ya uvunjivu wa amani.

Taasisi ya Global peace Foundation Tanzania imewataka vijana wa kitanzania kushiriki katika kulijenga taifa pindi wanapohitimu masomo yao wakiwa shule na vyuoni ili kuepuka kujiingiza katika matukio ya uvunjifu wa amani.

Global peace Foundation Tanzania  wakiendeleza mfululizo wa warsha zao za kuwajenga vijana leo wakishirikiana na kituo cha vijana wa Tandale Youth Development Center (TYDC)  kimeendelea kutoa warsha kwa kuwapa elimu vijana ya maisha baada ya shule.

Kamala Dickson kutoka Global peace Foundation akichangia jambo

Kamala Dickson mwanaharakati wa masuala ya vijana kutoka Global peace Foundation Tanzania amewataka vijana kuwa na mawazo chanya wakati wanapokuwa mashuleni, sababu vyanzo vya vijana kujiingiza katika matukio ya uvunjifu wa amani ikiwamo kujiingiza katika makundi ya kigaidi.

“Vijana wengi wakihitimu masomo yao wanakosa kujitambua kutokana na ugumu wa maisha uliopo hivyo kupelekea kuweza kushawishika na vikundi vya uvunjifu wa amani” Alisema.

Mmoja wa vijana ambao waliiudhuria katika mdahalo huo Mohamed Jafari alisema wanafunzi wakaiwa mashuleni fikra zao zainajengwa katika kuajiriwa pia kuchagua shughuli za kufanywa, “Vijana wanatakiwa wajamiiane na mazingira ya kawaida na wafanye shughuli mbalimbali”. Alisema.

Mohamed Jafari mmja kati ya vijana walioshiriki mdahalo

Tatizo la vijana kukosa jaira ni janga la kimataifa nchi nyingi zimekuwa zikikumbwa na lawama kutoka kwa serikali kushindwa kuwaandalia ajira vijana wengi wanaomaliza shule na vyuo.

Wengi wa wachangiaji walisema vijana wanatakiwa wajitambue, wasiwe wa binafsi na ubunifu, na kuondokana na akili za wengi zimeadumazwa fikra zao, na kukimbilia mijini.

Joseph Malekela miongoni mwa vijana ambao walishiriki na kuchangia kwamba vijana pindi wawapo shuleni wajitahidi kupitia na stadi za maisha.

“Vijana wanatakiwa wajitambue watoke kwenye fikra hasi kwenda chanya waelewe suala la ajira sio serikali tu wenyewe wanaweza kujiajiri na kufanya jamii kuwa yenye vijana wachapakazi na si wavunjivu wa amani” mmoja kati ya viongozi wa TYDC