Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Teddy Mapunda (wa tatu kulia) akizungumza katika makabidhiano ya vitabu vya Sheria ya Usalama Barabarani katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Trafiki jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, na kulia ni Meneja wa Mahusiano wa (SBL), Nandi Mwiyombela, huku kushoto ni Imani Lwinga Meneja wa Mawasiliano (SBL) na Inspekta A. B. Swai.