Na Sixmund Begashe wa Makumbusho ya Taifa
WATANZANIA wameshauriwa kuunga mkono jitihada mbali mbali zinazofanywa na Serikali, Mashirika ya Umma na Wadau mbali mbali katika mapambano dhidi ya rushwa ili kutokomeza kabisa tatizo hili hapa nchini.
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bwana ACHILES BUFURE kwenye usahili uliofanywa na Makumbusho hiyo ili kuchaguwa wasanii watakao unda kikundi kimoja kwa lengo la kutoa elimu ya Mapambano dhidi ya Rushwa hapa nchini.
Bw Bufure ameongeza kuwa Makumbusho imeona itumie wasanii wa fani mbali mbali kupitia program ya sanaa na Utamaduni ijulikanayo MUSEUM ART EXPLOSION ili kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi na ambao utakaokaa akilini mwa watu kwa muda mrefu kupitia sanaa za ufundi na zile za jukwaani.
Wakizungumza baada ya Usahili huo, msanii Bi Yame Muhamedi wa Kikundi cha sanaa cha UKOO na Salum Mbaya wa St Kamilius Wameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuwashirikisha wasanii katika program ya MUSEUM ART EXPLOSION AGAINST CORRUPTION kwani imewapa nguvu na hari ya kuendelea kufanya kazi za sanaa katika kuleta matokeo chanya ya kimaendeleo ndani ya nchi na kuahidi kufanya vyema kazi iliyopo mbele yao ya kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya madhara ya Rushwa nchini.
Program ya MUSEUM ART EXPLOSION AGAINST COTTUPTION ni moja kati ya program tano nchini zilizopata ufadhili wa Ubalozi wa Uswiss wenye lengo la kutoa elimu kwa watanzania juu ya Madhara na namna ya kupambana na Rushwa nchini.