BALOZI DK CHANA NA MWENYEKITI BODI YA LAPF WATEMBELEA BANDA LA LAPF SABASABA

Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dr. Pindi Chana akipokea zawadi kutoka kwa mtumishi wa LAPF Simboninsia Ndosi  alipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, kulia anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe.

 

Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dr. Pindi Chana akisalimiana na  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe alipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya LAPF Prof. Faustine Bee (katikati aliyeshika tuzo ya ushindi wa Lapf) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja masoko wa LAPF Bw. James Mlowe pamoja na wafanyakazi wa mfuko huo wakati alipotembelea banda la mfuko wa Pensheni wa LAPF katika viwanja vya Sabasaba.
Wanachama wapya wa LAPF wakielekezwa kujaza fomu ya kujiunga na mfuko huo mapema jana katika viwanja vya sabasaba.

 

Mtumishi wa LAPF  akimsajili  mmoja wa wanachama wa  LAPF alietembelea banda hilo.

 

Wateja wakiwa wanasubiri kupata kadi zao za uanachama mara baada ya kujiunga na mfuko huo katika maonesho ya sabasaba.

 

Maafisa wa LAPF wakitoa maelezo kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye banda la LAPF na kujiunga na uanachama kwenye mfuko katika maonesho ya SabaSaba.