Na Janeth Mushi, Arusha
BAADHI ya viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wamelazimika kwenda eneo lililozuka mapigano baina ya Wasonjo na Wamasai kijijini Kisiwasuwi na Olorieni Magaidulu, Wilaya ya Ngorongoro kudhibiti ghasia na mapigano yaliozuka eneo hilo. Akizungumza leo mjini hapa Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo, Leonard Paul, amesema wameondoka arusha mchana huu kuelekea eneo hilo.
Akitoa ufafanuzi zaidi muda mfupi kabla ya kuanza safari hiyo, amesema kwa taarifa walizopokea ni kwamba; mapigano hayo yalizuka Oktoba 10
mwaka huu na hadia sasa yamesababisha vifo vya vijana wawili wa kabila la Wasonjo.
Ameongeza tukio hilo lilitoke majira ya saa sita mchana na kuwataja waliofariki kuwa ni Elifa Genduli (19) mkazi wa Ngongomatere,
aliyepigwa risasi katika kiganja cha mkono na Mletwai Geswai (18) aliyepigwa risasi mgongoni katika mapigano hayo.
Amesema chanzo cha mapigano ni kugombea eneo la kulishia mifugo yao linalojulikana kwa jina la Olorieni Magaidulu, ambapo alisema kuwa eneo hilo limekwua na mgogoro wa muda mrefu wa kugombe a ardhi hiyo kati ya kabila hizo mbili huku kila upande ukidai kumiliki eneo hilo.
Paul amedai baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya pande hizo, walikubaliana eneo hilo libaki hivyohivyo na kila upande kutoingiza mifigo yao kwa lengo la kuwalisha mpaka eneo hilo litakapogawanywa kwa mujibu wa sheria.
Amesema pamoja na makubaliano hayo siku ya tukio vijana wawili wa kabila la Wasonjo waliingia katika eneo hilo na kuanza kuchunga mbuzi hali iliyoleta mtafaruku mkubwa kati yao na Wamasai na kuzuka mabishano ya muda mrefu hadi kundi la Wamasai lilipoanza kuwapiga risasi vijana hao na kufariki papo hapo.
Aidha amebainisha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wanakijiji
wanafanya msako mkali kuwatafuta kundi hilo la Wamasai waliohusika katika tukio hilo, kutokana na baada ya mauaji hayo kutokea hali ya usalama ilibadilika ghafla, na miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Waso ikisubiri taratibu za maziko.
WAKATI huo huo Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia Mlinzi wa
Benki Kuu tawia la Arusha Maombi Andrea Lusanda (48) kwa tuhuma za
kumuua kwa kutumia risasi dereva wa pikipiki aliyefahamika kwa jina la
Goodluck Joel(29).
Alisema kuwa mlinzi huyo alimwua dereva huyo kwa kutumia bastola
iliyokuwa na namba T. 7394-09D00311. Kaimu huyo alisema kwua tukio hilo lilitokea Oktoba 11 mwaka huu, majira ya saa 7.00 usiku, ambapo mlinzi huyo aliondoka lindoni na kwenda kunywa pombe eneo la Sanawari, kwenye Bar ya Prosela.
Alisema kuwa mlinzi huyo alikwenda chooni kujisaidia na aliporejea
ghafla alipopigwa na kitu chenye kitu uzito kichwani hali
iliyomsababisha kuanguka chini. Alisema baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa alinyanyuka na kumpiga risasi marehemu ambaye alikuwa akipata kinywaji katika baa hiyo na kusababisha mauti hapo hapo, huku akidhaniwa kuwa ndiye aliyehusika kumpiga.