Mbunge Halima Mdee Mikononi mwa Polisi Dar…!

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee

 

HATIMAYE Jeshi la Polisi Dar es Salaam limemkamata Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) ikiwa ni kuitikia amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Alli Hapi. Taarifa zinasema mbunge huyo, alikamatwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake Makongo Juu na anashikiliwa na Kituoni cha Polisi Oysterbay.

Kiongozi wa CHADEMA (Katibu) wa Dar es Salaam, Henry Kilewo ametoa taarifa za kukamatwa kwa Halima Mdee. Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amethibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Hapi jana aliliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumweka ndani saa 48 Mbunge Halima Mdee kwa madai kwamba kauli yake aliyoitoa akizungumza na wanahabari hivi karibuni ni ya kichochezi na inamfedhehesha, Rais John Pombe Magufuli.