Masikini Mdee, Polisi Waagizwa Kumkamata Saa 48

Mbunge wa Kawe, Bi. Halima Mdee

 

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Ally Hapi amelitaka Jeshi la Polisi Tanzania, kumtia ndani Mbunge wa Kawe, Bi. Halima Mdee kwa kile alichodai katoa kauli ya kumtusi, dhihaka na uchochezi kwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli katika kauli yake aliyoitoa kwa waandishi wa habari.

DC Hapi alisema kauli za mbunge huyo aziwezi kuvumiliwa hivyo kutaka akamatwa na atiwe ndani saa 48, akihojiwa na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria dhidi ya maneno aliyoyatoa jana Makao Makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam. Hapi aliongeza kuwa maneno aliyoyatoa Mbunge huyo ni matusi yenye lengo la kuleta uchochezi ambao unaweza kuhatarisha amani nchini.

“Sitamvumilia mwanasiasa yeyote atakayethubutu kutoa kauli za matusi dhidi ya Mh. Rais, au zenye kutaka kuleta uchochezi katika wilaya yangu.” alisema DC Hapi.