Mkurugenzi msaidizi nyanda za malisho kutoka wizara ya kilimo na Mifugo Bw. Victor Mwita (Kulia) ambaye alikuwa mwenyekiti wakati wa shughuli hiyo, akitoa mwongozo wa baadhi ya mambo.
Baadhi ya watumishi Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUP) wakiwa wanafuatilia kwa makini majadiliano hayo wakiwa mkoani Morogoro.
Mmoja wa wajumbe wa kikosi kazi hicho akichangia jambo wakati wa mjadala.
Bi. Amina Ndiko kutoka Shirika la kimataifa la Oxfam nchini Tanzania akitoa neno la shukurani mara baada ya kukamilisha zoezi la kukamilisha mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi.
Mratibu wa programu ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Care Bi. Mary Ndaro akizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo changamoto kubwa iliyopo inayochangia ucheleweshaji wa upimaji wa ardhi ni pamoja na kuwepo kwa bajeti ndogo.
Bw. Emanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Idara ya Misitu na Nyuki akichangia jambo wakati wa kukamilisha mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi.
Kikosi kazi wakiendelea na kazi ya majumuisho.
Bw. Zakaria Faustin Mratibu wa kitengo cha Ardhi na uwekezaji kutoka (TNRF) akizungumza jambo wakati wa majumuisho hayo.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kikosi kazi.
Kikosi Kazi cha Masuala ya Matumizi ya Ardhi kinachojumuisha wadau kutoka serikalini na asasi za kiraia wamekutana na
kukamilisha rasimu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya ardhi nchini. Mkakati itakayowasilishwa katika ngazi ya juu endapo utatekelezwa, kusimamiwa na kufatiliwa kwa umakini kwa asilimia kubwa nchi ya Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi zenye utulivu wa migogoro ya ardhi. Miongoni mwa wadau hao waliohudhuria katika kikao wapo kutoka taasisi za serikali na zisizo za serikali ikiwemo Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUP), Shirika la kimataifa la Care pamoja Shirika la Oxfam.

Akizungumza Mkoani Morogoro, Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUP)
Dk. Stephen Nindi alisema endapo rasimu hiyo itapitishwa na yale yaliyokuwepo ndani ya rasimu yakasimamiwa na kufatiliwa vizuri kwa kiasi kikubwa itawezesha vijiji na Wilaya kuwa na mpango mzuri wa matumizi bora ya Ardhi.

“Ndani ya rasimu hiyo imeweza kuchambua vizuri suala zima la matumizi ya Ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa itaondoa na kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi katika maeneo mengi ya nchi, baada ya rasimu hiyo kukamilika itaweza kupelekwa katika ngazi ya juu kwa ajili ya kupewa baraka na kuanza utekelezaji wake.” Alisema Dk. Nindi
Alisema kuwa kikosi kazi hicho kimeweza kutengeneza mipango ya ardhi takribani 100 kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kikosi kazi hicho kipipo undwa.
“Ile kazi ambayo tuliifanya kipindi kirefu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka Serikali na taasisi zisizo za kiserikali tangu mwaka jana kwa sasa imefikia katika hatua ya mwisho ya kuwasilishwa katika vyombo vya juu kwa lengo
la kupewa baraka ili utekelezaji wa jambo hilo liweze kuanza ,”alisema Dk. Nindi.
la kupewa baraka ili utekelezaji wa jambo hilo liweze kuanza ,”alisema Dk. Nindi.
Naye Mratibu wa programu ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Care Bi. Mary Ndaro alisema kuwa lengo kubwa la wao kukutana na wadau mbalimbali wa mipango ya matumizi bora ya ardhi ni pamoja na kuhakikisha kuwa kuna kasi ya upangaji wa ardhi katika nchi.
“Moja ya changamoto kubwa iliyopo inayochangia ucheleweshaji wa upimaji wa ardhi ni pamoja na kuwepo kwa bajeti ndogo. Maeneo mengi yakipimwa yanasaidia kuwepo kwa usalama wa miliki na hati miliki hususani kwa wananchi wa vijijini ambapo karibia asilimia 60 ya wananchi wanategemea ardhi kwa ajili ya kujipatia kipato hivyo kama nchi ni vema
kuwekeza katika upangaji wa matumizi ya ardhi ili kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi,” alisema Ndaro.
kuwekeza katika upangaji wa matumizi ya ardhi ili kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi,” alisema Ndaro.