UNIC yataka wahitimu Academic International kutojiingiza katika dawa za kulevya

Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo (kulia) na mgeni rasmi katika Maafali ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule ya Academic International (Academic International Primary School) ya jijini Dar es Salaam akiwasili katika ukumbi wa mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi ya Academic International, Bi. Natasha Karamagi akimuongoza mara baada ya kupokea heshima ya vijana wa Skauti shuleni hapo baada ya kupokewa.

 

Mgeni rasmi kwenye Mahafali ya wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Academic International (Academic International Primary School) na Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo (katikati) akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wahitimu wa darasa la saba kwenye hafla ya maafali hayo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa shule hiyo, Tom Bowyer.

 

Mgeni rasmi kwenye Maafali ya wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Academic International (Academic International Primary School) na Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi wahitimu wa darasa la saba aliofanya vizuri katika masomo yake. Wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa shule hiyo, Tom Bowyer pamoja na meza kuu wakishuhudia.

 

Picha ya baadhi ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule hiyo wakiwa na mgeni rasmi na viongozi wa Shule ya Academic International (Academic International Primary School) ya jijini Dar es Salaam.

 

Burudani ya ngoma ikitolewa na wanafunzi wa Shule ya Academic International (Academic International Primary School) katika hafla ya Maafali ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule hiyo.

 

Wanafunzi waliohitimu Darasa la Saba wa ‘Academic International Primary School’ wakiwa katika picha ya pamoja.

 

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wahitimu Darasa la Saba katika shule ya Academic International wakiwa katika hafla ya maafali hayo.

KITUO cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimewaonya wanafunzi wa ‘Academic International Primary School’ waliohitimu Darasa la Saba kutojiingiza katika dawa za kulevya, kwani ni eneo linaloharibu kwa kasi maisha ya vijana wengi kupitia makundi. Ushauri huo umetolewa jana na Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza na vijana hao wahitimu darasa la saba katika shule hiyo ya jijini Dar es Salaam.

Afisa huyo kutoka UNIC, Bi. Vuzo ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya mahafali hayo alisema wamekuwa na program ya kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya, wamebaini kuwa vijana wengi wanaotumia dawa za kulevya wamefuata mkumbo toka kwa marafiki zao na kwenye makundi na kupata madhara makubwa ikiwemo kuharibu maisha yao.

“Ukweli ni kwamba matumizi ya dawa za kulevya hayajaribiwi, ukianza tu matumizi ndio umeingia rasmi maana kiu ya kuendelea itakushinikiza. Vijana wengi wameharibu mustakabali wa maisha yao kabisa kwa madawa ya kulevya. Hii tu ni kwa kuwa walikosea katika kufanya maamuzi awali, walifanya maamuzi mabaya. Msikubali kutumika pia katika ubebaji madawa haya nje ya nchi kwa ahadi ya kupewa fedha nyingi au kazi nzuri. Msikubali kubeba mizigo ya watu hovyo mnaposafiri, mnaweza kujikuta mnaingia katika kesi ya kusafirisha madawa haya,” alisema Bi. Stella Vuzo akizungumza na wahitimu na wazazi wao.

 

Picha ya pamoja kati ya Meza Kuu na moja ya kikundi cha burudani cha wanafunzi wa Shule ya Academic International (Academic International Primary School) kwenye Maafali ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule hiyo ya jijini Dar es Salaam.

 

Picha ya pamoja kati ya Meza Kuu mgeni rasmi na baadhi ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule ya Academic International walioshinda tuzo mbalimbali za masomo.

 

Aidha aliwaeleza kuwa hatua wanaoingia ni ya kuchagua kuwa na marafiki wazuri ambao watakuwa mwongozo kwao na wasiogope kuzungumza nao juu ya changamoto mbalimbali zitakazo wakabili na kuangalia namna ya kuzitatua. Aliwahimiza kutambua kuwa kuanzia sasa wanaingia katika hatua ya mabadiliko kimaisha hivyo umakini unahitajika. “…Mnaingia kwenye hatua ambayo wewe mwenyewe utaanza kufanya maamuzi juu ya maisha yako. Si kitu kirahisi kama mnavyodhani umakini, nguvu na jitihada binafsi zinaitajika ili kujenga mustakabali wa maisha yenu.” Alisisitiza mgeni huyo rasmi kutoka UNIC.

“Bila shaka walimu hapa shuleni wamefanya kazi yao ipasavyo, kwa kuwafundisha na kuwasaidia katika masomo mbalimbali, Walimu wamewatia moyo na kuwapa motisha ili muweze kufanya vizuri katika mitihani yenu ya mwisho. Kwa upande wa wazazi wenu wamejitahidi kujitoa tangu mkiwa wadogo hata kuwasaidia kuwapa mazoezi madogo madogo nyumbani hadi leo hii ambapo mnaingia katika hatua nyingine ya maisha ya mwanadamu, hata hivyo kadri mnavyo endelea kukua mnatakiwa kuendana na tamaduni zetu za Kiafrika kuheshimu wakubwa zenu. Mnaitaji kuwa karibu na wazazi wenu na kuwasikiliza zaidi kuna mengi ya kujifunza kwao ambayo nyinyi hamna.”

Hata hivyo aliwataka kutambua kuwa kila hatua ya maamuzi wanayoifanya leo inaweza kujenga ama kuharibu maisha yao ya kesho, hivyo umakini zaidi unaitajika. Aliwataka wahitimu hao kutumia muda kujisomea vitabu, magazeti na machapisho mbalimbali ili kupata habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi na hata kujua nini kinaendelea nchini kwao na hata nje ya nchi.

“…Kuweni sehemu ya kutatua changamoto mbalimbali za ulimwengu. Muwe wabunifu na hata kuwasaidia wengine katika maisha mazuri. Msikubali kuingizwa katika tamaduni zisizofaa ama kupitwa na wakati. Teknolojia ni nzuri lakini msikubali kutekwa nayo, hata kuwaingiza katika mambo yenye madhara. Leo mnamaliza darasa la saba (std 7) ni hatua muhimu ya masomo, lakini huwezi kupata kazi kwa kutegemea cheti cha darasa la saba, endeleeni kusonga mbele kielemu.
Hakuna haja ya kupoteza muda “Fanya la wakati, wakati unawakati, kwani utakuja wakati utahitaji kufanya la wakati na hakutakuwa na wakati wa kufanya ya wakati”

 

Picha ya pamoja kati ya wahitimu wa Darasa la Saba na mgeni rasmi pamoja na Meza Kuu katika hafla ya maafali yao.

 

Picha ya pamoja kati ya Meza Kuu mgeni rasmi na baadhi ya wahitimu kumi bora waliofanya vizuri katika masomo yao.

 

Baadhi ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule ya Academic International wakiwa katika hafla ya maafali yao yaliofanyika shuleni hapo juzi.