Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua katika warsha iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kuwakutanisha wajumbe anuai kutoka asasi za kiraia kujadili bajeti kwa jicho la kijinsia. Warsha hiyo ya siku tatu inafanyika Ofisi za TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umekutanisha wawakilishi toka asasi mbalimbali za kiraia nchini kwa lengo la kuchambua bajeti kwa jicho la kijinsia. Akizungumza akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi alisema washiriki hao kwa pamoja washiriki hao wataangalia kila asasi inafanya nini katika kuichambua bajeti kwa mlengo wa kijinsia. “Tutajadilia na kuangalia kila asasi inafanya nini katika malengo endelevu ya kidunia, nani anafanya nini katika mkataba wa SADC, nani anafanya nini katika mkataba wa Afrika Mashariki kisha kuangalia pia tunakujaje kwa pamoja kushirikiana,” alisema Bi. Liundi.
Alisema katika warsha hiyo ya siku tatu washiriki pia wataangalia wajibu wa Serikali na jamii kiujumla katika kuendeleza ajenda ya Serikali ya uchumi wa viwanda, pamoja na kujadili utekelezaji wa bajeti kupitia sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, maji na afya na namna zinavyopewa kipaumbele. “…Tutaangalia pia Serikali wajibu wake ni nini, wananchi nao wajibu wao ni nini ili twende wote kwa pamoja. Tanzania ya viwanda ni yetu sote hivyo lazima tuwajibike kwa pamoja,” alisema Bi. Liundi.
Meneja wa Programu ya Ujenzi wa Vuguvugu la Harakati ya Kumkomboa Mwanamke, Grace Kisetu (kulia) na mratibu wa warsha hiyo akizungumza kutoa maelekezo kwa washiriki.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua katika warsha iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kuwakutanisha wajumbe anuai kutoka asasi za kiraia kujadili bajeti kwa jicho la kijinsia. Warsha hiyo ya siku tatu inafanyika Ofisi za TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa warsha iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kuwakutanisha wajumbe anuai kutoka asasi za kiraia kujadili bajeti kwa jicho la kijinsia wakifuatilia mada anuai. Warsha hiyo ya siku tatu inafanyika Ofisi za TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa washiriki wa warsha iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kuwakutanisha wajumbe anuai kutoka asasi za kiraia kujadili bajeti kwa jicho la kijinsia akichangia mada. Warsha hiyo ya siku tatu inafanyika Ofisi za TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.