TANZANIA inatarajia kunufaika na teknolojia ya kisasa ya usafirishaji ya Moovn Driver, kwa watu wanaohitaji kupiga simu ya mkononi kuhitaji usafiri. Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Godwin Ndugulile amesema huduma hiyo itawasaidia madereva wa taksi, pikipiki na bajaji nchi kufanya biashara kwa wakati na kukuza kipato chao na nchi kwa kulipa kodi ikiwa ni pamoja na kufanya huduma hiyo kuwa ya uaslama zaidi.
Amesema mtu atahitaji usafiri wa taxi au bodaboda, bajaji kwa nyakati tofauti ataweza kupata huduma hiyo kupitia teknolojia tuliyoibuni kupitia vijana mainjinia wa masuala ya Teknohama ambao ni watanzani wa hapa hapa nyumbani Tanzania na kupelekwa popote aendapo.
Ndugulile amesema kuwa dereva huyo kwa mfumo huo ataonekana kila sehemu atakapokwenda kupitia tekinolojia hii.
Amesema watumiaji satelaiti ambapo abiria atakapo kuwa akiitumia kumtafuta dereva itamuonesha dereva aliyekuwa karibu yake na kuongeza kuwa endapo dereva huyo naye atakuwa akiitumia atapata taarifa kuwa katika eneo Fulani kuna abiria.
Alisema aplikesheni hiyo inapatikana bure kwa wateja wote ili kuweza kutoa huduma nafuu kwa vyombo vya usafirishaji mbalimbali kama taxi bodaboda, na bajaji.
Amesema madereva wataongeza kipato, watarahiaisha biashara, usalama dhidi ya mteja aliyempakia, mawasiliano, ripoti ya mapato na malipo ya kirahisi ya kulipwa kwa njia ya mtandao kupitia teknolojia hiyo.
Wakati kampuni nyingine zinamkata dereva asilimia 25 mpaka 45 ya mapato ya siku na haziruhusu kupokea Bakshishi kutoka kwa mteja kampuni hiyo ya Moovn Driver itamkata dereva asilimia 15 tu ya mapato yote ya siku ikiwa ni pamoja na kumruhusu dereva kupokea tipu au (Bakshishi) kutoka kwa mteja.
Kabla ya kuanza kwa huduma hiyo serikali imeshirikishwa ambapo pia Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga alitaarifiwa kuhusu huduma hiyo ambayo italeta tija na manufaa kwa kupunguza uhalifu, uwezo wa kukusanya kodi sahihi ya mapato ya madereva na kuongeza kipato, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha madereva wanafuata sheria na vibali na kurahisisha ajira.
Ameongeza kwa kuwahamasisha madereva kujiunga na huduma hiyo ambayo itakuwa na faida kubwa kwao lakini pia itawafanya kuendesha kazi zao kwa usalama zaidi kwa kuwa watakuwa kwenye mfumo wa Setilaiti hivyo kuimarisha pia usalama wa wateja.