SBL Yatoa Zawadi ya Gari ya Milioni 50 kwa Msambazaji Bora

Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo (wa kwanza kushoto) akimkabidhi nyaraka za gari aina ya Heicher  lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika,  ambaye ni msambazaji wa kanda aliyeibuka msambazaji anayeongoza  katika kipindi cha kwanza cha nusu mwaka  huu wa fedha 2017.wanaoshuhudia katikati ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy ,na Baraka Kilimba Meneja Mauzo Baraka Kilimba na mwishoni ni Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha.

 

Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo Akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu zawadi ya msambazaji bora ambapo MM Group kutoka Mpanda aliibuka mshindi ,kulia kwake ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy na kushoto kwake ni Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika,mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

 

Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo wa kutangaza mshindi mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

 

Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kutangaza mshindi wa shindano la msambazaji bora ambapo MM Group toka Mpanda aliibuka mshindi ,anayefuatia katikati ni Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo na mwishoni kulia ni ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy ,mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

 

Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika akijaribu gari lake mara baada ya kukabidhiwa baada ya kuibuka kama msambazaji bora ,Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

 

Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari aina ya Heicher  lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imetoa zawadi ya gari aina ya Heicher  lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa MM Group,  ambaye ni msambazaji wa kanda aliyeibuka msambazaji anayeongoza  katika kipindi cha kwanza cha nusu mwaka  huu wa fedha 2017.
Kampuni ya MM Group ambayo  ina makao yake  wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi iliwashinda wasambazaji wengine 85 walioshiriki kwa ajili ya kupata zawadi hiyo  ya kipekee. Akiendesha  hafla hiyo ya makabidhiano  iliyofanyika katika makao makuu ya SBL Temeke, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo  alimpongeza mshindi  huku akithibitisha kujikita kwa kampuni  hiyo ya bia katika kutambua  juhudi zinazofanywa na wateja wake  katika kuunga mkono ukuaji kwa kampuni.
“Wakati tunapongeza  mchango wa MM Group kwa kuongoza na kushika nafasi ya juu  katika kipengele chake kulikomwezesha kupata zawadi hii, tunatambua pia  kazi nzuri inayofanywa na  wasambazaji wengine, wateja na hali kadhalika wadau wetu. Kupitia uungwaji mkono huu wa dhati, SBL imekua katika uzalishaji  na kufikia kiwango cha juu  katika sekta ya uzalishaji bia  ndani   ya nchi na hata katika ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema Tayo.
Akitoa wito kwa wasambazaji wengine wa SBL kuiga mfano wa MM Group, Tayo aliwahahakishia washirika wa SBL kibiashara wakiwamo wasambazaji na wateja kwamba SBL itaendelea kuwaenzi na kusikiliza mahitaji yao.
“Tunawashukuru wadau wetu wote kwa kuzingatia kwamba  wamekuwa pamoja nasi katika katika safari yetu ndefu na ya mafanikio kibiashara”, alibainisha Tayo.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika, wakati akiishukuru SBL kwa zawadi hiyo,  aliwapa changamoto wasambazaji wengine kuendesha na kuenenda na ukaribu wa SBL kwa kufanya kazi kwa bidiii ili kufuzu kwa ajili ya tuzo kama hiyo.
“Naishukuru sana SBL  kwa kuheshimu ahadi yake  na kunituza gari hili Heicher. Hili gari ni zana  muhimu katika biashara yangu ambayo itaniwezesha kukuza shughuli zangu za usambazaji wa bidhaa za SBL,” alisema Bw Joseph Chanika kwa bashasha.