SBL Yaidhamini Taifa Stars kwa bilioni 2.1

 


Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kulia) akimkabidhi Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) mfano wa hundi ya fedha iliyotolewa na kampuni ya SBL kwa Taifa Stars. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akishuhidia.

 

Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kushoto) pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) wakionesha nakala za mikataba mara baada ya makabidhino ya hundi ya fedha iliyotolewa na kampuni ya SBL kwa Taifa Stars. Katikati yao ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akishuhidia.

 

Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (wa pili kushoto) pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (wa pili kulia) wakionesha nakala za mikataba mara baada ya makabidhino ya hundi ya fedha iliyotolewa na kampuni ya SBL kwa Taifa Stars. Katikati yao ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akishuhidia.


*Ni mkatanba wa miaka mitatu mfululizo

KAMPUNI ya Bia Serengeti (SBL) leo imeingia mkataba wa mitatu na Shirikisho la Mipira wa Miguu Tanzania (TFF)  wa thamani ya shilingi bilioni 2.1  ambao unaifanya kuwa mdhamini  mkuu wa timu ya taifa -Taifa Stars.
Hii ni mara ya pili kwa SBL kuiunga mkono timu ya taifa baada ya kampuni hiyo kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu ilipoidhamini timu hiyo kati ya mwaka 2008 hadi 2011.
Katika makubaliano hayo ambayo yalisainiwa leo na pande hizo mbili na Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie na Rais wa TFF Jamal Malinzi, kampuni ya SBL itapata fursa ya kutanga biashara yake wakati wa mechi zote za Taifa Stars za nyumbani na ugenini.
Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo Bi Weesie alisema uamuzi wa kampuni hiyo wa kuidhamini timu ya taifa unatokana na sera ya SBL ya kusaidia kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo.
ga mkono sekta ya michezo nchini na kubainisha kwamba  michezo sio tu inaburudisha bali pia inaunganisha mashabiki na pia ni chanzo cha kipato kwa vijana.
“SBL inaona fahari kuidhamini timu yetu ya taifa kwa mara nyingine. Tumechukua hatua hiii kwa kuwa tunaelewa mchango wa sekta michezo katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aidha tunaamini kuwa udhamini wetu utachangia kukuza vipaji vya vijana wetu pamoja na kuleta hamasa kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya taifa,” alisema Weesie.

Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (wa kwanza kushoto waliokaa) pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (wa kwanza kulia) wakisaini mikataba hiyo ya kampuni ya SBL kudhamini Taifa Stars. Katikati yao ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akishuhidia.

 

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza kuishukuru SBL. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie.

 

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza kuishukuru SBL. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie.

Kwa upande wake, Rais wa TFF aliishukuru SBL kwa kukubali kuidhamini Taifa Stars jambo ambalo alisema litasaidia katika kufanikisha maandalizi mazuri na ushiriki kikamilifu wa timu hiyo katika mashindano mbalimbali, ndani nan je ya nchi.
“Udhamini wa SBL umekuja kwa wakati mwafaka, wakati ambapo timu yetu ya taifa ipo katika hatua za maandalizi kwa mashindano ya kikanda na kimataifa,” alisema Malinzi.
Hafla ya kusainiwa kwa udhamini huo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe ambaye  alitoa wito kwa  kampuni zingine na watu binafsi wenye mapenzi na michezo kujitokeza na kutoa michango ya hali na mali ili kuendeleza sekta hiyo.

Mkurugenziwa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha akizungumza katika hafla hiyo.

 

Viongozi mbalimbali wa wizara na TFF wakiwa katika hafla hiyo.