JUZI nilikuwa safarini kwa kazi za kijamii Mkoa wa Tanga. Miongoni mwa maeneo ambayo niliyatembelea ni Wilaya ya Korogwe ambayo ipo mkoani Tanga. Baada ya shughuli za kijamii niliamua kuvinjari baadhi ya mitaa kujua masuala anuai ndani ya mji huo.
Nikiwa kwa mbali niliona mkusanyiko wa watu eneo moja hivyo kuamua kujisogeza kujua kulikoni ndipo nikasogea na kukuta ilikuwa ni foleni ya kawaida eneo la Benki ya NMB. Wateja walikuwa wamepanga foleni wakisubiri kuingia katika mashine maalumu ambazo hutumika kwa kutolea fedha maarufu kwa jina la ‘ATM’.
Nilizungumza na baadhi yao wakadai hilo ni tukio la kawaida Wilayani hapo. Bahati mbaya sikubahatika kuwapata wahusika kutoa ufafanuzi ni kwanini kulikuwa na feleni takribani tatu kwa wateja jambo ambalo lilikuwa na usumbufu.
Lakini nikaona si vibaya kupata kumbukumbu kwa wasomaji wangu juu ya adha ya foleni katika mabenki ikiwemo hii. Wahusika vipi, fedha tuitafute kwa shida hata tukitaka kuitumia iwe hivyo hivyo! Duh.