Maadhimisho Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Maeneo Anuai

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubiwa wakati wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani huadhimishwa kila mwaka mwezi wa mei 3, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipitia ratiba ya hafla ya Kongomano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wqa Vyombo Vya Habari Duniani yaliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar.
Mc wa Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Ndg Suleiman Seif akitowa maelezo la kongamano hilo la kuadhimisha lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar.
Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Ndg Chande Omar akitoa maelezo wakati wa maadhimishi ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani ilioadhimishwa Zanzibar katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Kajubi Mukajanga akitowa maelezo wakati wa Kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar.
Wageni waalikwa na Viongogozi wa Vyombo vya habari Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Habari Tanzania Hassan Abdallah Mitawi akitowa maelezo ya hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutowa machache na kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuhutubia Kongamano hilo la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud akitowa nasaha zake wakati wa kongamano hilo kabla ya kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuhutubia hadhara hiyo ya waandishi wa habari mbalimbali walioko Zanzibar.

 

 

 

Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Ndg Chane Omar akiwasilisha Mada ya
kuhusu Umakini wa Fikra kwa wakati muhimu Nafasi ya Vyombo vha Habari katika
Kuimarisha jamii zenye Amani, Haki na Ujumuishwaji, wakati wa kongamano hilo la
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Chuo
cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar
MHADHIRI
wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Ndg Ali Uki akitowa Mada kuhusiana Uchambuzi wa
Sheria za Habari Zanzibar wakati wa Kongamano hilo.

 

 

MWANDISHI
wa Habari Muandamizi Ndg Enzi Talib akichangia mada zilizowakilishwa wakati wa
Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani
lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar

Makamu wa Pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya habari Zanzibar.
Katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC), Mei 3,2017 imefanya mkutano na wadau wa habari mkoani Shinyanga kujadili namna klabu hiyo ilivyo na wajibu wa kuendeleza amani katika jamii.
Mgeni rasmi katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel mjini Shinyanga alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack aliyekuwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga.

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari huadhimishwa duniani kote kila ifikapo tarehe 3 mwezi Mei ya kila mwaka ambapo pamoja na maadhimisho ya kitaifa kufanyika kitaifa jijini Mwanza,lakini yamefanyika pia katika kila mkoa nchini yakiwa na kauli mbiu inayosemayo “Klabu za Waandishi wa Habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii”.

Awali akitoa hotuba yake,Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde alisema Klabu za waandishi wa habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii hivyo kuwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao vizuri kuandika habari zinazojenga utaifa na kuleta mshikamano katika jamii.

Malunde alisema Klabu za waandishi zinawaweka pamoja waandishi wa habari hivyo kupitia umoja huo zinawabijika kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza amani katika jamii kwani pasipo na amani hakuna maendeleo.
Aliongeza kuwa kutokana na nguvu ya vyombo vya habari,amani katika jamii itaendelea kuwepo endapo tu waandishi wa habari watazingatia maadili ya kazi yao na kuepuka kushabikia mambo yasiyo na maana.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack aliwataka waandishi wa habari kutanguliza utanzania na uzalendo katika habari wanazoandika.

“Ndugu zangu waandishi wa habari mnajukumu kubwa la kulinda amani ya nchi hii,tumieni kalamu zenu vizuri,epukeni kuandika habari za kujenga hofu na mnapoandika basi msiegemee upande mmoja,sikilizeni hata upande wa pili ili kutenda haki”,alieleza mkuu wa mkoa.

Katika hatua nyingine Telack aliwahamasisha waandishi wa habari kuimarisha mshikamano walionao na kujiendeleza kielimu huku akiwashauri kuanzisha miradi itayowakomboa kiuchumi kwani fursa mbalimbali za kiuchumi zipo mkoani humo.

“Nitoe wito kwa waandishi wa habari kuunga mkono sera ya uchumi wa viwanda,andikeni habari kuhusu viwanda na kilimo na kupitia umoja wenu anzisheni mashamba ya pamba na alizeti na mnao uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo ili kuinua uchumi wenu,andikeni proposal mnaweza kuanzisha hata kiwanda cha maziwa”,aliongeza Telack.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack akifungua mkutano wa wadau wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ngazi ya mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack. Kushoto ni Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro.Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde.
Katikati ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack.
Wa kwanza kulia ni  Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani akifuatiwa na Kanali Mussa Kingai ambaye ni mwakilishi wa vikosi JWTZ Shinyanga kwenye kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa habari mkoa wa Shinyanga kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani Mei 3,2017.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akitoa hotuba ukumbini.
Wadau wa habari wakiwa ukumbini
Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Stephen Wang’anyi akisisitiza jambo ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mwandishi wa habari Suleiman Shagata akichangia hoja ukumbini.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akiongoza majadiliano ukumbini.
Kaimu Mwenyeti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Shaaban Alley akizungumza ukumbini.
Mratibu wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Nunu Abdul akiandika dondoo muhimu.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Mkutano unaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Kamanda  wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza ukumbini.
Msaidizi wa Askofu Kanisa kuu la KKKT Shinyanga Usharika wa Ebenezer Trafaina  Assery Nkya akizungumza ukumbini.
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire akizungumza ukumbini.
Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani akizungumza ukumbini.
Kanali Mussa Kingai ambaye ni mwakilishi wa vikosi JWTZ Shinyanga kwenye kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga akichangia hoja ukumbini.
Mdau Gelard Ng’ong’a kutoka shirika la Rafiki SDO.
Afisa habari kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mji wa Kahama (KUWASA) , Mkama akichangia hoja.
Bwana John Myola kutoka Shirika la AGAPE Shinyanga akizungumza ukumbini.
Mkurugenzi Msaidizi Radio Faraja,bwana Anikazi Kumbemba akizungumza ukumbini.
Mwakilishi wa Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Bi Alice Mazoko akichangia hoja.
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack,wadau wa habari na waandishi wa habari.
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack,wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga na waandishi wa habari. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi akifungua maadhimisho ya
siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani kimkoa yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga (Tanga Press Club)
leo kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani
Tanga,Hassan Hashim kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi
wa Habari Mkoani Tanga, Lulu George.

 

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga, Hassan Hashim akizungumza katika maadhimisho hayo leo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga, Lulu George
akizungumza katika maadhimisho hayo kushoto ni Katibu Msaidizi Alex
Abraham.

 

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga, Hassan Hashim kushoto
akifurahia jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi
mara baada ya kupokea cheti  cha kuripoti habari za majanga na hali
hatarishi jana mafunzo waliyoyapata mkoani Morogoro hivi karibuni katika
halfa iliyofanyika.

 

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga, Lulu George
naye akipokea cheti hicho kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benedict Wakulyamba kulia ni 
Mwenyekiti wa Klabu
ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga, Hassan Hashim.

 

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya
Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Amina Omari naye akipokea cheti
hicho
Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari
na Mwandishi wa Clous TV Mkoani Tanga Zawadi Kika naye akipokea
cheti
Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari
na mwandishi wa gazeti la Citizen Paskal Mbunga naye akipokea
cheti
Mmiliki
wa Blog ya Tanga Kumekucha na Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa
habari mkoani Tanga,Salum Mohamed naye akipokea cheti
hicho
 Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji
Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorah Killo
akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo
Kamanda
wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi
Benedict Wakulyamba akizungumza jambo kwenye maadhimisho
hayo
Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
akizungumza umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na
fursa zinazopatikana kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tanga Press
Klabu,Lulu George
Afisa Uchunguzi kutoka Takukuru Mkoani
Tanga,Frank Mapunda akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo
leo
Afisa
kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia
akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo kulia ni Meneja wa Mfuko huo
Mkoani Tanga,Ally Mwakababu anayefuatia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya
Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Club) Lulu
George
 Sehemu ya waandishi wa habari
mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo leo

 

  Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo leo.

 

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF),Ally Mwakababu kulia akiteta jambo na
Mwandishi wa gazeti la Mtanzania katikati Amina Omari kushoto ni Ofisa wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia

Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Klabu)Neema Omary kulia na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo,Amina Omari wakifuatilia matukio
mbalimbai
KATIBU Tawala Mkoa Tanga Mhandisi Zena Said ameziagiza taasisi za Serikali na mashirika ya umma kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapohitaji taarifa kutoka kwenye taasisi hizo kwa ajili ya kuhabarisha umma.

 

Ameyazungumza hayo leo wakati wa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani ambapo Mkoa Tanga maazimisho hayo yalifanyika katika ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari na kuhudhuriwa na
wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na zisizo za kiserikali.

 

Hatua hiyo imekuja mara baada ya waandishi wa habari kutoa malalamiko yao mbele ya Katibu Tawala huyo wa Mkoa ambae alikua mgeni rasmi katika maazimisho hayo ya kuwa zipo baadhi ya taasisi za Serikali kushindwa
kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapohitaji kutekeleza majuku yao ya kazi.

 

Burhan Yakubu ambae ni mjumbe na mwaandishi wa habari  alisema kumekuwepo na utaratibu usioendana na maadili ya kiuwandishi katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Bombo kwa kutengeneza urasimu wa kupatikana kibali kutoka kwa katibu tawala Mkoa wakati mwandishi anapohitaji kupatiwa tariifa zozote kutoka katika Hospitali
hiyo

 

“Tumekuwa tukikwama kutekeleza wajibu wetu hasa tunapohitaji kupata taarifa katika Kuu ya Rufaa ya Bombo na kulazimishwa mpaka tupate kibali kutoka kwa katibu Tawala jambo ambalo limekuwa liktkwamisha katika shughuli
zetu”Alisema Yakubu.

lea ufafanuzi malalamiko hayo Mhandisi Zena  alisema taasisi zote zinapaswa kutambua kuwa wanahabari wanahaki ya kupatiwa taarifa sahihi kwa lengo la kuihabarisha jamii na hakuna sababu za kuweka vikwazo kwao kwa lengo la kuwakwamisha kutimiza majukumu yao.

Mhandisi Zena alisema zimekuwepo taarifa za malalamiko kwa waandishi kuwa zipo baadhi ya tasisi kama Hospitali ya Rufaa ya Bombo kutokutoa ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa habari pindi wanapotaka kutekeleza
wajibu wao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

 

“Tusiwawekee mipaka waandishi wakati wanapotaka kutekeleza majuku yao na tayari nimekwisha toa agizo sio Hospitali ya Bombo tu hili ni kwa taasisi zote,hakuna jambo linaloweza kufanyika na mwananchi akaweza kulipata
kwa wakati ikiwa hakuna waandishi,tunatambua umuhimu wenu na thamani yenu ni kubwa kwa Taifa Hili.”Alisema

 

Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao vema na kuwepo na maadili yatakayokuwa na maslahi mapana kwa ajili ya amani ya nchi na kujiepusha na taarifa zitakazoweza kuliingiza Taifa
kwenye machafuko.

 

Katika hatua nyingine Mwandishi wa Tanzania Daima Mkoani Tanga Mbaruku Yusuph alitaka kupatiwa ufafanuzi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga,Kamishna Msaidiz,Mwandamizi wa Polisi Benedict Wakulyamba,juu ya
usalama wa waandishi wa habari wanapotekeleza wajibu wao hasa katika mikutano ya kisiasa.
Mbaruku alisema hivi karibuni kumeripotiwa kutokea matukio kwa baadhi ya waandishi wa habari maeneo mbalimbali hapa nchini kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kushindwa kuwajibika katika harakati zao za kupata
habari kwa lengo la kuhabarisha umma na kujenga hofu kubwa kwa baadhi yao juu ya usala wa maisha yao.

 

Kamanda wakulya alisema jukumu la usalama lipo mikononi mwa jeshi hilo na wajibu wa polisi kutambua uwepo wa waandishi na umuhimu wao katika kila tukio ambapo alitoa rai kwa waandishi hao kuziona dalili za uvunjifu wa amani na kuanza kujiepusha mapema kabla ya madhara makubwa hayaja tokea.