YALIYOJIRI MAADHIMISHO YA ‘MEI MOSI’ VIWANJA VYA USHIRIKA MOSHI, KILIMANJARO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wafanyakazi katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitabasamu wakati Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi wakiwa katika maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo nchini yamefanyika Kitaifa katika Chuo cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi wakiwa wanapita mbele yake kwa njia ya maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo nchini yamefanyika Kitaifa katika Chuo cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki pamoja na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya.

 

Sehemu ya Wafanyakazi waliofika kwenye Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

 

Sehemu ya Wafanyakazi waliofika kwenye Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono wakati wa wimbo wa Mshikamano daima pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki, Rais wa Shirikisho la Vyama vya vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Saidik.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono wakati wa wimbo wa Mshikamano daima pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki, Rais wa Shirikisho la Vyama vya vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Saidik.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akitoa salamu za Mkoa kwenye Sikukuu hiyo ya Wafanyakazi Duniani.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akitoa salamu katika Sikukuu ya Wafanyakazi mkoani Kilimanjaro.

 

DONDOO ZA VIONGOZI KATIKA SHEREHE HIZO
#Tunakushukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo suala la elimu bure nchini – Said Meck Sadik.

#Kati ya walimu wa Sayansi 100 waliopangikiwa mkoa wa Kilimanjaro, 94 wamesharipoti – Said Meck Sadik.

#Serikali ya Mkoa imekuwa ikisisitiza uanzishwaji wa mabaraza ya wafanyakazi mahala pa kazi – Said Meck Sadik.

# Changamoto ya ukosefu wa ajira ni la tatizo la Dunia na Tanzania ni moja ya nchi inayokabiliwa na tatizo hilo – Mkurugenzi ILO.

#Kwa jitihada zinazofanywa na serikali, tunaona uchumi wa kati uko karibu – Mkurugenzi ILO.

# Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kazi kwa ukaribu na TUCTA na ATE – Jenista Mhagama.

#Tucta inaishauri Serikali kufuata sheria za kazi katika kuwachukulia hatua wafanyakazi – Dkt. Yahaya Msigwa.

#Tunaishauri Serikali kuharakisha uboreshaji wa mifuko ya jamii ili wafanyakazi waanze kunufaika – Dkt. Yahaya Msigwa.

#Wapo waajiri ambao wanakiuka sheria za kazi, mfano kunyanyasa watumishi na kutoa kazi kwa ndugu zao – Dkt. Yahaya Msigwa.

#Tunaiomba Serikali kupandisha kima cha chini cha mshahara unaokatwa kodi kufikia 750,000/-. – Dkt. Yahaya Msigwa.

#Tucta inawakumbusha wafanyakazi kutimiza wajibu wao sehemu za kazi – Dkt. Yahaya Msigwa.

#Si wajibu wa Tucta kutetea uovu kama vile ulevi, ubadhilifu na utoro sehemu za kazi – Dkt. Yahaya Msigwa.

#Tunaipongeza Serikali kwa kusisitiza uanzishwaji wa mabaraza ya wafanyakazi katika maeneo ya kazi – Dkt. Yahaya Msigwa.

#Tunakushukuru Mhe. Rais kwa kubali kuwa mgeni wetu rasmi wa siku hii ya leo – Tumaini Nyamhokwa – Rais TUCTA.

#Siku ya Wafanyakazi Duniani ni siku muhimu kwa wafanyakazi kutafakari masuala yanayowahusu – Rais Magufuli.

#Wafanyakazi ndio injini ya maendeleo katika taifa lolote duniani – Rais Magufuli.

#Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zinazowakabili wafanyakazi – Rais Magufuli.

#Nawahakikishia wafanyakazi kuwa tunaanza ukurasa mpya kwani serikali tumeamua kwenda mbele – Rais Magufuli.

#Nawaarifu kuwa serikali inaendelea na utaratibu wa kuanzisha fao la Bima ya Ajira na wadau wameshatoa maoni – Rais Magufuli.

#Serikali inalishughulikia suala la ucheleweshaji wa mafao ili wafanyakazi wanapostaafu waache kuhangaika – Rais Magufuli.

#Vyama vya Wafanyakazi ni mahala pa kazi na sio hiari na visigeuzwe sehemu ya migogoro – Rais Magufuli.

#Waajiri wote wanatakiwa watoe mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kinyume na hapo ni kuvunja sheria – Rais Magufuli.

#Serikali itaendelea kusaini na kuridhia mikataba ya kimataifa wafanyakazi yenye maslahi kwa wafanyakazi – Rais Magufuli.

#TUCTA endeleeni kuwaelimisha wafanyakazi ili fedha za bodi ya mikopo ya elimu ya juu ikusanywe kikamilifu – Rais Magufuli

#Tumebaini watumishi hewa 19706 waliokuwa wanaisababishia serikali hasara ya Tsh Bil. 230 kwa mwaka katika misharaha peke yake – Rais Magufuli.

#Serikali itashughulikia suala la mfumuko wa bei ili kuondokana na ugumu wa maisha – Rais Magufuli.

#Wapo walio na umri wa kustaafu lakini hawataki kuondoka hawa nao tutaanza kuwafuatilia, hawana tofauti na watumishi hewa – Rais Magufuli

#Nilitaka nisafishe kwanza kabla ya kupandisha mishahara kwa wafanyakazi ili tusiwafaidishe wasiostahili – Rais Magufuli.

#Nawaahidi tutatoa ajira 52000 katika sekta mbalimbali baada ya kutoa watumishi hewa na walio na vyeti feki – Rais Magufuli.

#Yeyote atakayehamishwa hakuna kuhama mpaka ulipwe hela ya kuhamishwa – Rais Magufuli.

#Serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wafanyakazi na haitadharau wala kupuuza maombi yenu – Rais Magufuli

#Niwaahidi wafanyakazi kuanzia bajeti ijayo tutaongeza mishahara kutoka kiwango kilichokaa kwa muda mrefu – Rais Magufuli.

#Mwaka huu tutapandisha madaraja ya kazi pamoja na kuweka nyongeza ya mishahara kuwa sawa na madaraja yake – Rais Magufuli.

#Serikali hii itakuwa mtetezi namba moja kwa wafanyakazi – Rais Magufuli.

#Nikitoka hapa nitakaa na Baraza la Mawaziri ili kuweka mikakati ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi – Rais Magufuli.

#Kwa sheria zote zitakazoletwa kama miswada tutafanyia kazi kwa wakati ili mambo yenu yaende vizuri – Spika Job Ndugai

#Nasisitiza msiwahamishe wafanyakazi kabla hamjawalipa stahili zao – Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO