Na Mwandishi Wetu
ZIKIWA zimesalia siku nne kabla ya ratiba ya Ligi Kuu Daraja la Kwanza kuanza timu ya soka ya 94KJ yenye maskani yake Uwanja wa Vinyago Mwenge jijini Dar es Salaam inaendelea na maandalizi yake kwa kucheza mechi za kirafiki, ambapo tayari wiki hii imecheza mechi za kujipima nguvu.
Siku ya Jumanne timu hiyo ilishuka dimbani katika Uwanja wa Vinyago Mwenge kupima nguvu na timu ya Kijitonyama Stars na kuishinda magoli manne kwa mawili wafungaji wa magoli ya 94KJ yaliwekwa kimyani na Godfrey Danda, Dani Mepya, Joseph Mhagama, na Edward Kheri wakati magoli ya Kijitonyama Stars yalifungwa na Mahmoud Mahadhi akifunga magoli yote mawili.
Mechi ya pili ambayo wamecheza jana dhidi ya timu ya Ikudu na kufanikiwa kuifunga timu hiyo kwa idadi ile ile ya magoli manne kwa mawili, mawili 94KJ yamefungwa na Joseph Mhagama wakati magoli mengine mawili yamefungwa na Godfrey Danda na Said Achimwene.
Kwa mijubu wa kocha mkuu wa timu giyo mwinyimadi tambaza amesema wanafanya maandalizi ya mwisho kabla ya kupangwa kwa ratiba ili kujiweka sawa na ligi hiyo inayoatajia kuanza oktoba kumi na tano ambapo timu hiyo ipo kundi C pamoja na timu za Ausha football club, Polisi Morogoro, Polisi Tabora, Rhino Rangers, Tabora, na Samaria ya Iringa.
Timu hiyo ya 94KJ imeshawakilisha wachezaji wake wa usajiri katika Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) na imekwisha lipa ada ya Ushiriki ya mashindano shiringi laki mbili. Kwa mawasiliano Mwinyimadi Tambaza 0715923561 na ni mwenyekiti wa chama cha kuendeleza mpira kwa watoto chini ya miaka kumi na saba (KIDIYOSA).