Na Mwandishi Wetu, Arusha
ALIYEKUWA Naibu Meya wa Jiji la Arusha na diwani wa kata ya Kimandolu, Estomih Mallah amevunja ukimya na kumtaka Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa na viongozi wenzake kuacha kuwadanganya wananchi wa Arusha na Watanzania kuhusu sakata la umeya wa Arusha kwa madai kuwa hakuna tena njia ya kumtengua nafasi hiyo meya wa CCM, Gaudance Lyimo aliyepo madarakani.
Kupitia taarifa aliyotoa kwa vyombo vya habari leo jijini hapa, Mallah
aliwaeleza wandishi wa habari kuwa na siku 30 za kisheria za kufungua
shauri mahakamani la kumpinga meya huyo kupitishwa, Dk. Slaa alikuwa na taarifa kuhusu muafaka huo na aliubariki.
Alisema siku ya kikao cha mwisho cha muafaka huo Dk. Slaa alituma
ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi kupitia kwa Katibu wa Chadema mkoa, Amani Golugwa majira ya saa 6:25 na sekunde 43 uliosomeka, “Please nimeongea na Dk. mkimaliza itumwe taarifa nzima ya kikao hicho leo ila muendelee kutupa what is going on msije mkachemsha”.
Alisema kutokana na ujumbe huo ambao haukuwaelekeza waishie wapi au kuachana na kikao hicho hali ambayo iliwapa wao madiwani waliokuwa katika kikao hicho kufikia maamuzi waliliyoyafikia na kwamba alipeleka taarifa ya kikao hicho siku hiyo hiyo kwa Dk. Slaa kama alivyoelekezwa ili kuitafuta na kuilinda amani ya Mji wa Arusha.
Aliwaonya vijana na wananchi mbalimbali wanaoshabikia jambo hilo kuwa pindi vurugu itakapotokea hawataka kuwa na mahali pa kukimbilia zaidi ya vijijini mwao walikotokea wakiwa na suruali na mashati yao katika mifuko ya nailoni kwa kuhofia kudhurika na vurugu hizo.
Aliongeza kuwa vurugu kwa kiasi kikubwa zinaonekana kuchochewa zaidi
na watu wa nje ya mkoa wa Arusha ambao hufika hapa wakati wa maandamano mbalimbali ambayo huwagombanisha wao kwa wao na kisha kuelekea majimboni kwao kufanya kazi za maendeleo na wao kubaki na malumbano yasiyo ya msingi.
Mallah alidai kuwa yeye na madiwani wenzake wanne waliovuliwa uanachama na CHADEMA, hawana ugomvi na kiongozi yeyote wa Chadema na ndiyo maana pindi walipopatiwa taarifa ya kuvuliwa uanachama walikimbilia mahakamani na sio kumfuata kiongozi yeyote ili kudai kurejeshewa uanachama wao.
Alitumia fursa hiyo kukionya Chadema na kukitahadharisha kuwa kimejaa watu wanafiki, wachochezi na wachonganishi na kwamba wakiachiwa kuendelea kukaa katika chama hicho watakisambaratisha na kushindwa kuonesha upinzani wa kweli bali wa kinafiki na hatimaye anguko la aibu la chama hicho.
Aidha Mallaha alisisitiza kumtambua Meya aliyepo madarakani kwa hivi
sasa kwa madia kwua amechaguliwa kihalali katika uchaguzi uliofanyika
mnamo Desemba 18 na madiwani wa vyama vyote na kisha kufikiwa muafaka baada ya vurugu za kutomtambua mnamo mwezi Juni mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mallah, alisema kuwa kwa hivi sasa wanko katika mchakato wa kufungua kesi upya ya kudai kurejeshewa uanachama waliovuliwa ikiwa ni baada ya Makahaka ya hakimu Mkazi mkoani Arusha kuifuta kesi hiyo ikiwa ni pamoja na kudai kwua Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo, huku akidai kuwa hadi hivi sasa hakuna chombo chochote cha sheria kilichotoa barua ya kutenguliwa kwao katika nyadhifa za udiwani.
Hakimu wa Mkazi wa Mahakama hiyo, aliyekuwa akisikiliza shauri hilo
Hawa Mguruta akitupilia mbali kesi hiyo mahakamani hapo alisema kwua
mahakama hiyo haiwezi uingilia maamuzi ya Kamati Kuu ya (CHADEMA)
ambapo chama hicho kimesajiliwa kisheria kama chama cha siasa hivyo
maamuzi waliyoyatoa kwenye chama hicho ni sahihi.
Mguruta alidai kuwa Mahakama hiyo haiwezi kukiuka katiba ya chama
hicho pamoja na maamuzi yote yaliyofikiwa huku akinukuu kesi
mbalimbali ziliwahi kuamuliwa na mahakama mbalimbali nchini.
Wakili wa upande wa utetezi Method Kimomogolo katika kesi hiyo, moja ya
pingamizi zake alizoziwasilisha mahakamani kwa njia ya maandishi
alidai kuwa kutokana na madiwani hao kukata rufaa Baraza Kuu la Chama
hicho na Mahakama haina uwezo wa kusikiliza kasi hiyo bali Mahakama Kuu
pekee ndiyo yenye uwezo, pingamizi ambazo Mguruta alikubaliana nayo na
kuitupilia mbali kesi hiyo.