Jacob Zuma Awatumbua Mawaziri, Yumo Waziri wa Fedha

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.

RAIS wa nchi ya Afrika Kusini, Jacob Zuma amewafukuza kazi mawaziri wake kadhaa akiwemo Waziri wa Fedha, Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio wanaotajwa kulazimika kwake kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri. Taarifa zilizopatikana kutoka Ikulu ya nchi ya Afrika Kusini zinaeleza kuwa tayari, Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Fedha wa taifa hilo kwa sasa.

Takriban mawaziri 15 wametimuliwa katika serikali ya Zuma jambo ambalo limekuwa likizua mjadala mkubwa kwa wachambuzi wa masuala ya kisiasa kimataifa.
-BBC