KUTANGAZWA kuuzwa kwa hisa za kampuni ya Mawasiliano ya Vodcom kumeendelea kutoa hamasa kwa watu binafsi na makundi mbalimbali kuendelea kununua hisa za kampuni hiyo, Benki ya Covenant imeendelea kujikita kuwahamashisha vikundi vya wanawake kujiunga na kununua hisa za kampuni hiyo badala ya kuvunja vikundi vyao na kugawana fedha.
Akizungumza katika Hafla ya uzinduzi wa kikundi cha VICOBA cha Mabibo Farasi kununua hisa za Vodacom, Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, Amesema umefik wakati sasa vikundi hivyo kuacha utaratibu wa kuvunja vikundi vyao kila inapofika mwisho wa mwaka ili kujikita katika kufanya uwekezaji, hasa wa kununua hisa.
“Ninawasihi wanawake na vikundi vingine vyote kuacha utaratibu wa kuvunja vikundi vyao na kugawana pesa, bali wajikite katika kufanya uwekezaji kwa kununua hisa za kampuni ya Vodacom ambazo zimewekezwa kwa mara ya kwanza nkatika soko la hisa ambazo endapo watanunua katika kipindi hiki watakuwa na nafasi ya kutengeneza faida kubwa,” Alisema Mwambenja na Kuongeza.
“Hii ni fursa kubwa kwa wanawake hasa walio katika vikundi kujikita kufanya uwekezaji katika soko la hisa, Covenant Bank tumeshirikiana na Zan Securities kuweza kuwawezesha wajasiriamali wadogo pamoja na vikundi vingine kuweza kununua hisa za Vodacom,” Alihitimisha Mwambenja.
Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi wenzake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Mabibo Farasi Grace Ngonyani amesema wameamua kuachana na utaratibu wa Kuvunja kikundi kila inapofika mwisho wa mwaka na kujikita katika uwekezaji ili waweze kupata faida zaidi, Pamoja na kukata bima ya Matibabu kwa Familia zao.
Hii karibuni benki hiyo iliungana na Kampuni ya Uwakala wa Soko la Hisa ya Zan Securities, ili kuviwezesha vikundi vya wajasiriamali wadogo kuweza kujiunga na kununua hisa za awali za kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom ambazo zimeingizwa sokoni mapema mwezi huu.