Hivi Ndivyo Tundu Lissu Alivyoshinda Urais wa Chama cha Wanasheria, TLS

WAKILI msomi Mhe. Tundu Lissu ameibuka na ushindi wa Urais wa Chama cha Wanasheria Nchini (TLS) baada ya kujizolea kura 1,411 kati ya 1,682 zilizopigwa, ikiwa ni sawa na 88% ya kura zote. Uchaguzi huo ulifanyika Arusha International Conference Centre (AICC).

“Nimeshinda Urais TLS, ushindi huu uende kwa watanzania wote, na kwa wote mlioonewa ambao mpo mahabusu na magerezani” alisema Tundu Lissu. Wakati Lissu akitwaa nafasi hiyo, upande wa nafasi ya Makamu wa Rais imekwenda kwa wakili Godwin Ngwilimi.

Nafasi ya Uraisi wa TLS iligombewa na wajumbe;
1. VICTORIA MANDARI
2. FRANCIS STOLLA
3. LAU KEGO MASHA (ambaye alijitoa na kuungana na Tundu Lissu)
4. GODWIN MWAPONGO
5. TUNDU LISSU

Wajumbe wa Baraza la TLS waliochaguliwa ni pamoja na;
1. Jeremiah Mtobesya
2. Gida Lambaji
3. Hussein Mtembwa
4. Aisha Sinda
5. Steven Axweso
6. David Shilatu
7. Daniel Bushele