Umoja wa Mataifa kupitia Mkurugenzi wake Mkazi nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez umetembelea, kukagua na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na umoja huo Mkoani Kagera ambapo zaidi ya Dola za Kimarekani (618,000 USD) zimetolewa ili kufadhili na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama Elimu na Afya pia na miradi ya kijamii.
Bw. Alvaro Rodriguez ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Mashirika matatu ya Umoja wa Maifa nchini Tanzania (IOM, UNICEF na UNDP) aliwasili Mkoani Kagera Machi 13, 2017 na ujumbe wake ili
kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo na Kijamii inayofadhiliwa na Umoja huo katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.
kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo na Kijamii inayofadhiliwa na Umoja huo katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.
Miradi aliyoitembelea Bw. Rodriguez ni pamoja na mradi wa ujenzi wa vyoo, madarasa, mabweni na jengo la utawala katika shule ya Msingi Mgeza Mseto Manispaa ya Bukoba ambapo mara baada ya kukamilika mradi utagharimu Dola za Kimarekani (318,000 USD) ambapo ujenzi wa vyoo umekamilika, madarasa mabweni na jengo la Utawala ujenzi upo katika hatua ya msingi.
Bw. Rodriguez akiongea na wanafunzi, walimu na wananchi waliofika kumpokea katika shule hiyo alisema kuwa amefurahishwa kufika katika shule hiyo na kujionea hali halisi ya watoto wenye ulemavu wa albinizimu na walemavu wengine aidha, alisema kuwa Umoja wa Mataifa uliamua kutoa fedha hizo ili kurejesha miundombinu ya shule hiyo baada ya kuharibiwa na etemeko la Ardhi lilitokea Septemba 10, 2016.
“Nilipokuwa Dar es Salaam niliambiwa na Waziri Profesa Joyce Ndalichako kuwa nikifika Kagera nitembelee Shule ya Msingi Mugeza Mseto pia nilipofika Kagera Mkuu wa Mkoa ameniambia nitembelee shule hii sasa nimejionea na kujua ni kwanini walinisistiza, shule inahitaji msaada
mkubwa.
mkubwa.
Aidha, Umoja wa Mataifa unapenda kusaidia lakini Tanzania shule za namna hii zipo nyingi na ndiyo maana tunasaidia kidogo kidogo ili kuongeza mahitaji muhimu.” Alisistiza Bw. Rodriguez
Pai Bw. Rodriguez alisema kuwa mara baada ya kujionea hali halisi ya shule hiyo ataendelea kushawishi wafadhili mbalimbali ili kuhakikisha shule hiyo yenye mahitaji maalum inapewa kipaumbele katika ufadhili.
Vilevile aliiomba jamii kutowanyanyapaa watoto wenye ulemavu kwani ulemavu hauna ukabila, utaifa wala rangi ambapo alisema kuwa hata yeye watoto wake ni walemavu jambo ambalo alisema ulemavu hauna mzungu wala mweusi.
Umoja wa Maifa pia umetoa ufadhili dola za Kimarekani (250,000 USD) kwenye shule za Msingi 16 Katika Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ili kujenga vyoo na kuimarisha mifumo ya maji kwa ajili ya uboreshaji wa usafi na mazingira. Pia kukarabati
miundombinu yote iliyoharibiwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea mwaka jana 2016.
miundombinu yote iliyoharibiwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea mwaka jana 2016.
Ukaguzi wa Miradi mbalimbali iliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Maifa pia umetoa ufadhili dola za Kimarekani (250,000 USD) kwenye shule za Msingi 16 Katika Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ili kujenga vyoo na kuimarisha mifumo ya maji kwa ajili ya uboreshaji wa usafi na mazingira. Pia kukarabati
miundombinu yote iliyoharibiwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea mwaka jana 2016.
miundombinu yote iliyoharibiwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea mwaka jana 2016.
Aidha, Umoja wa mataifa kupitia Shirika lake la (UNICEF) ulitoa ufadhili wa kujenga majiko sanifu katika jamii kwa ajili ya kutunza mazingira kwa wananchi wa hali ya chini kwa kutumia nishati ya kuni kidogo. Pia kupitia shirika la (IOM) wananchi na kaya masikini waliokumbwa na Tetemeko
la Ardhi mwaka 2016 waligawiwa vifaa mbalimbali kama ndoo, magodoro, blanketi, bati, vyandarua na vifaa vya kujengea makazi ya muda katika Halmashauri za Bukoba Manispaa, Bukoba na Missenyi.
la Ardhi mwaka 2016 waligawiwa vifaa mbalimbali kama ndoo, magodoro, blanketi, bati, vyandarua na vifaa vya kujengea makazi ya muda katika Halmashauri za Bukoba Manispaa, Bukoba na Missenyi.
Katika Hatua nyingine Bw. Rodriguez alikagua mradi uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa wa kufunga umeme wa jua katika Zahanati ya Bushasha Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Shule ya St. Mary Rubya Seminari Wilayani Muleba. Katika Shule ya Rubya Seminari ufungaji wa umeme wa jua uligharimu Dola za Kimarekani (50,000 USD) hadi kukamilika.
Baadhi ya watoto wa Shule ya Mugeza Mseto ilioyopo Bukoba Mkoani Kagera.
Akitoa maelezo ya Mradi huo Padre Malianus Rutagwerela ambaye ndiye Mkuu wa Seminari hiyo alisema kuwa mradi huo umeongeza nguvu ya mwanga katika shule hiyo na kuwa na umeme wa uhakika ikiwa ni pamoja na umeme wa TANESCO. Aidha aliushukuru umoja wa Mataifa kwa niaba ya uongozi wa Jimbo Katoliki la Bukoba kuwa mradi huo utaboresha zaidi elimu katika Seminari hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkazi Bw. Rodriguez alifurahishwa sana na mradi huo ambao alishuhudia ukifanya kazi vizuri. “ Nimefurahishwa na mradi huu pia sisi kama Umoja wa Mataifa tutaendelea kuona jinsi ya kusaidia shule kama hizi ili Mapadre na Viongozi wa dini waendelee kuzalishwa katika shule kama hizi ili wasaidie kueneza neno la Mungu kuhusu upendo na kuondoa chuki kati ya Wanadamu.
Alieleza Bw. Rodriguez kuwa amefurahishwa na utekelezaji wa miradi ambayo ipo chini ya Mashirika ya Umoja wa Maifa ambayo imetolewa ufadhili wa fedha na Umoja huo na kutekelezwa au inaendelea kutekelezwa Mkoani Kagera. Aidha, alihaidi kuendelea kuushawishi Umoja huo na wafahili mbalimbali ili waendelee kuuangalia na kuufadhili Mkoa wa Kagera katika miradi mbalimbali ya maendeleao na Kijamii.
Pichani kulia ni aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu .