RC Gambo Azinduwa Huduma ya TTCL 4G LTE Mkoani Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ‘RC’, Mrisho Gambo akizungumza alipokuwa akizinduwa huduma ya TTCL 4G LTE Mkoani Arusha.

Pichani ni Kaimu Afisa mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Wazir Kindamba, Akizungumzia mipango na mikakati wa TTCL.

Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifuatiwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL ,Wakipiga simu mubashara “live” kutoka Arusha kwenda Dar kwa kutumia laini mpya ya TTCL 4G LTE.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo Akihudumiwa na kupata maelekezo jinsi ya kutumia laini ya TTCL 4GLTE kutoka kwa mtoa huduma wa TTCL.


Kutoka kulia ni Mtendaji mkuu wa Huawei Tanzania Bw. Bruce, Akifuatiwa na Meneja wa TTCL Arusha Mh: Humphrey Ngowi,Anaefuatia ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Akifuatiwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba.

Habari/Picha na Imma Msumba, Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo Amezindua rasmi  huduma ya TTCL 4G LTE Mkoani  Arusha, Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu huyo wa Mkoa amesema,
“Nashukuru sana TTCL kwa kutuletea 4G LTE  Mkoani kwangu maana Arusha ni Jiji la Kimataifa kutokana na kuwa kituo kikuu cha Sekta ya Utalii katika eneo hili la Afrika Mashariki.

Pia Arusha ni Makao Makuu ya jumuia ya Afrika Mashariki, Soko la Kimataifa la Madini na vito vya thamani hasa Madini ya Tanzanite ambayo hayapatikani sehemu nyingine yoyote duniani, isipokuwa Mererani-Arusha-Tanzania.

Aidha, Arusha ni kituo kikubwa cha Kitaaluma hapa nchini kikiwa na idadi kubwa ya shule na Taasisi za Elimu, Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda na Shughuli nyingine nyingi za Kitaifa na kimataifa.”
“Hata hivyo Arusha pia ni Jiji kubwa la kibiashara na kituo kikubwa cha shughuli za kiuchumi kati ya Tanzania na Nchi jirani hasa Kenya, Uganda, Sudan na nchi nyingine. Katika jamii hii ya Mkoa wa Arusha yapo makundi yenye idadi kubwa ya watu kama vile Wanafunzi, Wafanyakazi wa Sekta mbali mbali, Wafanyabiashara na Wakulima ambao wote hawa, wanahitaji sana Mawasiliano ya uhakika na yenye tozo nafuu katika kufanikisha shughuli zao. Natumia fursa hii kukuhakikishia kwamba, Arusha ni soko la uhakika la bidhaa na huduma za TTCL. Tunachohitaji ni huduma bora za uhakika.”

Kadhalika Rc Gambo alisisitiza kwamba yeye atakuwa mstari wa mbele kwa kutumia huduma ya hiyo.

“mimi binafsi na Watendaji wote walio chini yangu, kutumia huduma za TTCL ili kuhamasisha wengine kuiunga mkono Kampuni hii ambayo ni mali ya Wananchi kwa asilimia mia moja.
nitalifikisha kwa wenzangu ili litengenezewe utaratibu mzuri wa utekelezaji. Ila mimi binafsi, tayari nimeshasajili namba yangu ya TTCL ambayo nitaanza kuitumia leo hii hapa mbele yenu wote mshuhudie.”