Waziri Prof. Makame Akagua Ujenzi Terminal III, JNIA

Mkuu wa timu ya usimamizi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam, Eng. Julius Ndyamukama (kushoto) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ramani ya miundombinu katika jengo hilo alipofanya ukaguzi mapema leo.

 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya BAM International inayojenga Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

 

Muonekano wa jengo la Tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi.