Rhino Cement Tanga Yasaidia Madawati 350 Shule ya Msingi Kange

Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rinho, Girish Kumar kimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa moja ya madawati 350 kwa shule ya msingi ya Kange  kupunguza kero ya uhaba
wa madawati kwa shule hiyo ambayo awali wanafunzi walikuwa wakisomea chini.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa, amekishukuru kiwanda cha Saruji cha Rhino cha Tanga kwa msaada wake wa madawati 350 kwa shule ya Msingi ya Kange na mabenchi 10 kwa Zahanati iliyopo ndani ya kata hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano, Mwalapwa alisema msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi darasani kukaa chini hivyo kutaka makampuni mengine kufuata nyayo za kiwanda hicho cha Rhino.
Amesema mabenchi 10 kwa Zahanati pia itaondosha kero kwa wagonjwa wanaofika kituoni na kuondosha kero ya foleni ya kukaa chini kusubiri
huduma.
“Niseme kutoka moyoni nimepata faraja kubwa kwa ndugu zetu
kutukumbuka jiwe moja kwa ndege wawili, madawati 350 kwa shule na mabenchi 10 kwa Zahanati, hili ni tukio jema la faraja” alisema Mwailapwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rhino, Girish
Gumar, amesema msaada huo wa madawati 350 na mabenchi kwa Zahanati uko na thamani zaidi ya milioni 45.
Alisema kiwanda cha Rhino kimekuwa kikisaidia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Afya, Mazingira na huduma nyengine za kijamii.  

 

 

 

 

 

 

 

 

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange  Tanga wakipeleka madawati madarasani kati ya madawati  350 yaliyotolewa  na kiwanda cha Saruji cha Rinho jana. Shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa madawati na baadhi ya wanafunzi kulazimika kukaa chini.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tangakumekucha.