RC Gambo Atembelea Nyumbani kwa Hayati Sokoine, Monduli

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, akisalimiana na Mjane wa Hayati Sokoine.

Na Imma Msumba, Monduli

MKUU wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo wikiendi hii alipata nafasi ya kutembelea nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine huko Monduli juu Wilayani Monduli.

Mh;Gambo alipata wasaaa wa kuzungumza na wajane wa kiongozi huyo mkubwa wa Kitaifa aliyefariki kwa ajali ya gari mwaka 1984 eneo la Dumila huko Mkoani Morogoro,

Mkuu wa mkoa alipata wasaa wakuzungumza na familia hiyo pamoja na wakazi majirani wanaozunguka  familia hiyo na kusema  maneno machache ambapo Alisema
“Kutembelea maeneo haya ambapo zipo kumbukumbu za mashujaa wetu waliolipigania Taifa letu kwa uzalendo mkuu inatusaidia sisi viongozi vijana kuzirudia hadhiri zetu za uongozi ili tuweze kuwatumikia wananchi wanyonge kwa Uadilifu na uwajibikajiili kuacha alama katika nafasi tulizopewa na kuwatumikia wananchi kama walivyofanya wazee wetu hawa.”

 

Kutoka Kulia ni Diwani wa Monduli juu akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli na pia ni Diwani wa Monduli Mjini Mh: Issack Joseph,Akisalimiana na Mjane wa Hayati Sokoine .

 

 

Mh: Gambo akiwa ameambatana na Mjane wa Sokoine Pamoja na watumishi mbalimbali wa Serikali,Wakitoa Heshima kwenye kaburi la Hayati Sokoine.
Mkuu wa mkoa wa Arusha  Mh: Mrisho Gambo  akipanda mti wa kumbukumbu nyumbani kwa Hayati Sokoine.Picha na Msumbanews.com